Protini

(Elekezwa kutoka Proteini)

Protini ni molekuli ndefu na sehemu za lazima katika muundo wa seli za mwili wa viumbehai. Zinajengwa na amino asidi. Protini huwajibika kwa maumbile ya seli na kushughulika usafirishaji wa dutu ndani ya seli na kati ya seli za mwili. Musuli zinaundwa pamoja na protini za pekee zenye uwezo wa kupanua na kujikaza hivyo kuweka msingi wa mwendo.

protein model mosaic.

Protini zinapatikana katika wanyama, mimea, fungi na bakteria.

Protini katika chakula

hariri

Wanyama wote pamoja na binadamu huhitaji protini katika chakula chao kwa sababu hawana uwezo wa kujitengenezea amino asidi zote zinazohitajika kwa kujenga miili yao. Kwa sababu hiyo tunahitaji chakula chenye protini; mahitaji ya mwanadamu ni takriban gramu 1 ya protini kwa kilogramu 1 ya uzito wa mwili wake; maana yake mtu mwenye uzito wa kilogramu 70 anashauriwa kula gramu 70 za protini kwa siku.

Tumboni mwa binadamu na wanyama protini za chakula huvunjwa kwa asidi asidi ndani yao; kutoka hizi mwili unajenga protini mpya ya aina yake ya pekee.

Uhaba wa protini unasababisha magonjwa; uhaba mkali unaleta unyafuzi. Unyafuzi unashika hasa watoto wanaopewa chakula kingi lakini kabohidrati tu kama ugali bila makundekunde, nyama au samaki.

Vyakula vyenye protini nyingi ni

Protini katika mlo nyongeza

hariri

Kando na chakula, protini huweza kupatikana katika mlo nyongeza (diet supplements). Kwa mfano whey protein ni mojawapo wa milo nyongeza ambao utaongeza mwili wako protini na kukuwezesha kutimua misuli.

Umuhimu wa protini katika mlo nyongeza

  • Husibisha na humfanya mtu ahisi amekinai na hivi kupunguza njaa
  • Hukuza misuli
  • Humsaidia mtu kukuwa sawa kwa haraka baada ya mazoezi
  • Hupunguza mafuta mwilini
  • Kumfanya mtu awe na uzani wa kawaida

Utaalamu

hariri

Protini zilitambuliwa na mwanakemia Msweden Berzelius mwaka 1838.

  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Protini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.