DNA ni kifupisho cha DeoxyriboNucleic Acid ambayo ni jina la Kiingereza la molekuli kubwa ndani ya seli za viumbehai wote. Kwa Kiswahili huitwa Asidi DeoksiriboNukleini (ADN kwa kifupi) au Asidi Kiinideoksiribo[1].

Mfano wa mfumo wa DNA.

Wanyama, mimea, bakteria na virusi vilevile, wote wana DNA. Molekuli hii inabeba ndani yake habari zote za urithi wa kiumbehai husika, yaani habari za tabia zote zinazopokelewa kutoka kwa wazazi. Mwenye DNA zimo jeni zinazotunza habari maalumu juu ya urithi wa kiumbe.

Molekuli ya DNA ina umbo kama ngazi mbili za kupanda zilizounganishwa pamoja na kupindika kama sukurubu. Kila ngazi ni nukleotidi ambayo ni muungo wa sukari fulani pamoja na moja kati ya besi ogania nne. Ufutano wa besi hizo unaamua namna ya kutengeneza protini wakati wa kujenga seli mpya.

DNA ina uwezo wa kujinakili. Wakati wa kuzaa DNA inajipasua katikati ya pande mbili za "ngazi" yake. Hivyo nusu "ngazi" ya upande wa mzazi mmoja inaungana na nusu "ngazi" ya mzazi mwingine.

Tabia kama ukubwa, rangi ya ngozi au nywele ziko kila moja mahali pake; zikiunganishwa za baba na mama, kemia inaamua ni upande gani wenye athira zaidi na hivyo utajitokeza kwa mtoto.

DNA inatokea hasa ndani ya kromosomu kwenye kiini cha seli.

TanbihiEdit

  1. Kamusi Sanifu ya Biolojia, Fizikia na Kemia iliyotolewa na TUKI inaandika "asidi kiinidioksiribo". Inapendekezwa kutumia -deoksi- badala ya -dioksi- kwa sababu kiambishi de- inamaanisha "bila" (bila oksijeni) ilhali di- inamaanisha "mbili".

Viungo vya NjeEdit