Kilimarondo ni kata ya Wilaya ya Nachingwea katika mkoa wa Lindi, Tanzania, yenye msimbo wa posta namba 65326[1].

Kata hiyo ina jumla ya vijiji vitatu ambavyo ni Namatunu, Nanjihi na Kilimarondo.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 6,717 [2]. Wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, idadi ya wakazi wa kata ilikadiriwa kuwa watu 4,509.[3] Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 4,344 [4] walioishi humo.

Asilimia kubwa ya wakazi wa kata ya Kilimarondo ni Wandonde, kabila ambalo lugha yake ya asili inaelekea kupotea katika uso wa dunia.

Shughuli kubwa ya uchumi kwa wakazi wa Kilimarondo ni kilimo cha mazao mchanganyiko.

Kilimarondo kuna parokia ya Kanisa Katoliki (Jimbo Katoliki la Lindi) ambayo ilianzishwa mwishoni mwa miaka ya 1940 na wamisionari Wazungu.

Marejeo hariri

  1. https://tcra.go.tz/services/publication-of-postcode-list Tanzania Postcode List
  2. https://www.nbs.go.tz/
  3. Makadirio ya Idadi ya Watu katika Majimbo ya Uchaguzi kwa Mwaka 2016, Tanzania Bara, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dar es Salaam April 2016, iliangaliwa Mei 2021
  4. "Sensa ya 2012, Lindi - Nachingwea DC". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-06-29. 
  Kata za Wilaya ya Nachingwea - Mkoa wa Lindi - Tanzania  

Boma | Chiola | Chiumbati Shuleni | Kiegei | Kilimanihewa | Kilimarondo | Kipara Mnero | Kipara Mtua | Lionja | Marambo | Matekwe | Mbondo | Mchonda | Mitumbati | Mkoka | Mkotokuyana | Mnero Miembeni | Mnero Ngongo | Mpiruka | Mtua | Nachingwea Mjini | Naipanga | Naipingo | Namapwia | Namatula | Nambambo | Namikango | Nang'ondo | Nangowe | Nditi | Ndomoni | Ngunichile | Raha leo | Ruponda | Stesheni | Ugawaji


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Lindi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kilimarondo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.