Kima
Kima buluu
Kima buluu
Uainishaji wa kisayansi
Domeni: Eukaryota (Viumbe walio na seli zenye kiini)
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Primates (Wanyama wanaofanana kiasi na binadamu)
Nusuoda: Haplorrhini (Wanyama wanaofanana zaidi na kima)
Oda ya chini: Simiiformes (Wanyama kama kima)
Ngazi za chini

Oda ndogo 2:

Kima ni mamalia yeyote wa hali ya juu katika familia ya juu Cercopithecoidea (kima wa Dunia ya Kale) na oda ndogo Platyrrhini (Kima wa Dunia Mpya), kwa hivyo kima wa juu wasio Prosimii (nusuoda ya zamani) au masokwe na nyani. Kuna takriban spishi 264 wanaofahamika wa kima wanaowakilisha kundi kubwa la mamalia wa hali ya juu. Kima huonwa kama ni mwenye akili sana na tofauti na masokwe; kima daima huwa na mkia. Kima wa Dunia ya Kale wanafanana zaidi na masokwe kuliko kima wa Dunia Mpya.

Dume mdogo wa Kapuchini Paji-jeupe (Cebus albifrons)

Tabia hariri

Kima wana ukubwa tofauti kutoka milimita za urefu 140 – 160 (pamoja na mkia) na uzito wa gramu 120 mpaka 140, mpaka urefu wa mita moja wa kilo 35. Wachache huishi kwenye miti wakati mwingine huishi kwenye savana. Chakula chao ni matunda, majani, mbegu, maua, mayai na wanyama wadogo (ikijumuishwa wadudu na buibui).

Kima wote wa Dunia Mpya wana mikia tofauti na wa Dunia ya Kale. Baadhi ya kima wana uoni wa rangi na wengine hawana. Huku kima wa Dunia Mpya wakiwa na macho kwa mbele walionekana tofauti hata baina yao hasa pua, mashavu na sehemu ya nyuma kwa ujumla.

Uainishaji hariri

 
Kima-kindi
 
Kaku mlakaa katika Uthai

Ifuatayo ni orodha ikionesha familia za kima.

ODA PRIMATES
Nusuoda Strepsirrhini: komba, koni na lemuri
Nusuoda Haplorrhini
Oda ya chini Tarsiiformes
Familia Tarsiidae: komba vidole-virefu
Oda ya chini Simiiformes: kima
Oda ndogo Platyrrhini: kima wa Dunia Mpya
Familia Cebidae
Familia Aotidae
Familia Pitheciidae
Familia Atelidae
Oda ndogo Catarrhini: kima wa Dunia ya Kale
Familia ya juu Cercopithecoidea
Familia Cercopithecidae: kima, ngedere, mbega, makaku na nyani
Familia ya juu Hominoidea
Familia Hylobatidae: masokwe wadogo
Familia Hominidae: masokwe wakubwa na binadamu

Mahusiano na binadamu hariri

Spishi tofauti za kima wana mahusiano na binadamu, baadhi yao hufugwa kama wanyama wa nyumbani na hutumika kama kifani cha binadamu kwenye maabara na safari ya angani. Pia huwahudumia binadamu wenye udhaifu. Kuna baadhi ya kima huonekana kama wanyama waharibifu wa mazao.[1] Kima ambao pia wapo kwenye mbuga ya watalii lakini hugeuka kama kitishio kwa watalii huona kama kuna kikwazo kwa binadamu hivyo tatizo dogo.

Kwenye dini huwakilisha werevu.

Kama huduma kwa watu wasiojiweza hariri

Baadhi ya mashirika yamekuwa yakiwafunza kima wa wakapuchini kama wasaidizi kuwasaidia watu wenye matatizo ya uti wa mgongo na matatizo mengine ya kutembea. Baada ya mafunzo kutosha kima hawa huweza kuwahudumia barabara walemavu wakiwa ndani ya nyumba, kima husaidia kupika, kuosha uso na kufungua chupa za vinywaji.

Kwenye tafiti hariri

 
Kima wa maabara katika kizimba cha kampuni Covance huko Vienna, Virginia, 2004–05

Kima aina ya Macaques wale wa Afrika Green Monkeys, hutumika kwenye tafiti nyingi aidha kwa kukamatwa porini au kulazimishwa. Hutumika sana kutokana na uwezo wao mkubwa wa kubeba vitu, kuzaliana kwa muda mfupi na kufanana kwao sana kisaikolojia na kimaumbile na binadamu.

Angani hariri

 
Sam, kaku-rhesus, alirushwa angani, umbali wa maili 55 (89 km) na NASA katika 1959.

Nchi nyingi zinawatumia kima kama sehemu yao ya tafiti za anga kujumuisha Marekani na Ufaransa. Kima wa kwanza kwenda angani aliitwa Albert II, ambaye aliruka angani na roketi ya Marekani, mnamo Juni 14, 1949.

Kama chakula hariri

Ubongo wa kima unaliwa kama chakula kitamu huko Asia ya Kusini, China na Afrika.[2] Kwa taratibu ya dini ya kiislamu kula nyani ni marufuku kabisa. Hata hivyo kima huliwa sehemu nyingine za Afrika, ambako nyama yake huuzwa kama nyama ya msituni.

Tanbihi hariri

  1. doi:10.1023/A:1005481605637
    This citation will be automatically completed in the next few minutes. You can jump the queue or expand by hand
  2. Bonné, J. (2005-10-28). "Some bravery as a side dish". msnbc.com. Iliwekwa mnamo 2009-08-15. 

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.