Sokwe
Ngagi
Uainishaji wa kisayansi
Domeni: Eukaryota (Viumbe walio na seli zenye kiini)
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Primates (Wanyama wanaofanana kiasi na binadamu)
Nusuoda: Haplorrhini (Wanyama wanaofanana zaidi na kima)
Oda ya chini: Simiiformes (Wanyama kama kima)
Familia ya juu: Hominoidea (Masokwe)
Familia: Hominidae (Masokwe wakubwa)
Ngazi za chini

Jenasi 4:

Sokwe mkubwa au sokwe peke yake ni jina la binadamu na nyani wakubwa wa familia Hominidae wanaofanana sana na binadamu. Tofauti na nyani wengine ni kuwepo kwa mkia; karibu nyani wote huwa na mkia lakini masokwe wakubwa hawana kabisa. Binadamu (Homo) anahesabiwa pia kama jenasi yenye spishi moja katika familia hii.

Eneo na uenezaji

hariri

Masokwe wasiokuwa wanadamu wanaishi katika maeneo ya tropiki ya Afrika (masokwe mtu na ngagi) na Asia (orangutanu). Wote ni wakazi wa misitu ila tu masokwe mtu wanaoingia pia kwenye mbuga au savana. Wanadamu wanaishi duniani kote kwa kubadili mazingira yao, kuvaa nguo na kujenga majumba yanayowalinda kutoka joto kali ama baridi.

Spishi zilizokwisha

hariri

Lua error in package.lua at line 80: module 'Module:Navbar/configuration' not found.

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sokwe (Hominidae) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.