Kimolo (au El Molo) ni lugha ya Kiafrika-Kiasia nchini Kenya inayozungumzwa na Wamolo. Isichanganywe na lugha ya Kimolo inayozungumzwa nchini Sudan. Mwaka wa 1994 idadi ya wasemaji wa Kimolo imehesabiwa kuwa watu wanane tu; hata hivyo kuna Wamolo takriban 700 (2007) lakini wengi wameacha lugha yao na huongea Kisamburu au Kiturkana badala yake. Kwa hiyo, lugha ya Kimolo imekaribia kutoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimolo iko katika kundi la Kikushi.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kimolo (Kenya) kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.