Kinyama-kidoto
Kinyama-kidoto | ||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Koloni ya vinyama-kidoto kutoka Merikani (Barentsia laxa)
| ||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||
| ||||||||
Ngazi za chini | ||||||||
Familia 4:
|
Vinyama-kidoto ni wanyama wadogo wa maji wa faila Entoprocta walio na mwili kwa umbo la kidoto kwenye mwisho wa kikonyo kinamo. Wanafanana na kuhusiana na vinyama-kigoga na kwa kawaida huishi kwenye makoloni kama hawa.
Wanyama hawa huwa na ukubwa wa mm 0.1-7 bila kuhesabu kikonyo. Wana "taji" ya minyiri ambayo silio zao husababisha mikondo ya maji inayochota chembe za chakula kuelekea mdomo. Mdomo na mkundu yote miwili huwamo ndani ya "taji", kinyume na vinyama-kigoga (Ectoprocta) ambao wana mkundu nje ya "taji". Takriban spishi zote za vinyama-kidoto huishi katika makoloni ambayo yameunganishwa kwenye uso wa chini kama miamba, makombe, miani au majengo ya chini ya maji. Spishi nyingine huishi peke yao juu ya wanyama wengine wanaokula kwa kusababisha mikondo ya maji, kama vile sifongo-bahari, vinyama-kigoga au anelidi wanaokaa chini. Baadhi ya spishi hizi zinaweza kusonga polepole. Spishi 150 zote hutokea baharini, isipokuwa spishi mbili zinazoishi katika maji tamu.