Kisabaki ni lugha za Kibantu jamii ya Kiswahili zilizopewa jina la Mto Sabaki. Lugha za Kisabaki, mbali ya Kiswahili, zinahusisha Ilwana (Malakote) na Pokomo kwenye Mto Tana nchini Kenya; Mijikenda, inayozungumzwa katika pwani ya Kenya; Kikomoro, katika Visiwa vya Komoro; na Mwani, inayozungumzwa kaskazini mwa Msumbiji[1].

Katika uainishaji wa lugha wa Guthrie, Kiswahili kiko katika eneo la Kibantu G, ambapo lugha nyingine za Kisabaki ziko katika ukanda E70, kwa kawaida chini ya jina Kinyika, kama ifuatavyo:

  • Ilwana (Malakote) (E.701)
  • Pokomo (E.71)
  • Mijikenda (E.72–73) (kasikazini (Nyika), Segeju, Digo, Degere)
  • Comorian katika makundi mawili, Magharibi (Shimwali na Shingazidja) na Mashariki (Shimaore na Shindzwani)
  • Mwani (Msumbbiji)
  • Makwe Swahili (Brava, Somalia), Coastal Swahili (Lamu, Mombasa, Zanzibar), Pemba Swahili (Pemba, Mafia)

Kwa kuongeza, kuna krioli na pijini kadhaa za Kiswahili: Cutchi-Swahili, Kiswahili), Kikeya.Kingereza, Sheng, Shaba kiswahili (Katanga Swahili, Lubumbashi Swahili), Ngwana (Congo kiswahili), Kikeya.

Marejeo

hariri
  1. Derek Nurse & Thomas J. Hinnebusch, 1993, Swahili and Sabaki: a linguistic history.