Kisangir ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia na Ufilipino inayozungumzwa na Wasangir kwenye visiwa vya Sangir, Mindanao, Balut na Sarangani. Mwaka wa 1993 idadi ya wasemaji wa Kisangir nchini Indonesia imehesabiwa kuwa watu 200,000, na mwaka wa 1981 kumehesabika wasemaji 55,000 nchini Ufilipino. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kisangir iko katika kundi la Kifilipino. Kisangir na lugha ya Kisangil nchini Ufilipino huelewana hadi wataalamu wengine wameziangalia lugha hizo kuwa lahaja za lugha moja tu.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kisangir kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.