Mindanao ni kisiwa kikubwa cha pili katika Ufilipino ambayo ni nchi ya visiwa. Eneo la visiwa ni 97,530 km² kuna wakazi milioni 22. Mji mkubwa ni Davao yenye wakazi milioni 1.5.

Ramani ya Mindanao
Wavuvi wa Mindanao

Jina hili latumiwa pia kutaja kundi la visiwa vya Ufilipino linayojumlisha kisiwa kikubwa cha Mindanao pamoja na funguvisiwa ya Sulu.

JiografiaEdit

Mindanao ni kisiwa ambacho kipo upande wa mashariki kabisa wa eneo la Ufilipino na karibu zaidi na Borneo. Asili ya kisiwa hiki kama Ufilipino wote ni ya kivolkeno; ni sehemu ya milima ya kivolkeno iliyokua kuanzia vilindi vya bahari juu ya "pete la moto" kando la bamba la Pasifiki.

Uso wa Mindanao ni ufuatano wa safu za milima na mabonde kati yao. Magma na majivu ya kivolkeno zilijaza mabonde kadhaa na kuwa nyanda za juu zenya sehemu za tambarare. Pwani huwa pia vipande vbya tambarare vinavyokatwakatwa na milima inayoelekea hadi katika baharini.

Mlima mkubwa ni Apo unaofikia kimo cha mita 2,954, ni pia mlima mkubwa wa Ufilipino. Kuna malighafi nyingi ambazo bado hazikutumiwa kiuchumi kutokana na ugumu wa mawasiliano na hali ya kisiasa kisiwani hasa uhaba wa usalkama kutokana na uasi wa wakazi Waislamu dhidi mya serikali.

WakaziEdit

Wakazi wanatumia lugha mbalimbali. Watu wa kusini ya kisiwa ni zaidi Waislamu walio theluthi 1 ya wakazi wa Mindanao. Sehemu kubwa zaidi ya 60% ni Wakristo hasa Wakatoliki. Vikundi vidogo vilitunza dini na tamaduni asilia.