Kisukari
Kisukari fedha (Ariomma bondi)
Kisukari fedha (Ariomma bondi)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii (Samaki walio na mapezi yenye tindi)
Oda: Perciformes (Samaki kama ngege)
Familia: Ariommatidae (Samaki walio na nasaba na visukari)
Haedrich, 1967
Jenasi: Ariomma
Jordan & Snyder, 1904
Ngazi za chini

Spishi 7, 2 katika Afrika ya Mashariki:

Visukari au haluwa ni samaki wadogo hadi wastani wa baharini wa jenasi Ariomma, jenasi pekee ya familia Ariommatidae katika oda Perciformes, wanaotokea maji ya kina kikubwa.

Pezimgongo la visukari limegawanyika katika mapezi mawili. Lile la mbele lina miiba 10-12 na lile la nyuma lina tindi 14-18. Kuna mikuku minono miwili kila upande wa msingi wa mkia. Urefu wao ni sm 20-35 na kipeo cha sm 80 (kisukari mapezi-mafupi).

Hula gegereka wadogo na planktoni wanyama.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za Afrika

hariri

Marejeo

hariri
  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kisukari (samaki) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.