Mifano
  • Yeye 'ndiye mwalimu wao
  • Sisi tu wanafunzi watiifu
  • Jembe li shambani

Kitenzi kishirikishi (alama yake ya kiisimu ni: t) ni kitenzi ambacho hujulisha hali ya kuwepo au kutokuwepo kwa uhusiano/ushirikiano baina ya vipashio vya lugha. Uhusiano huo unaweza kuwa katika tabia, hali, au mazingira fulani.

Mfano

  • Khadija ni mwizi (ni, ni hali ya kuyakinisha ya kwamba Khadija ana uhusiano na tabia ya wizi).
  • Joseph alikuwa mwalimu wetu (tendo kamilifu).
  • Amina hakuwa mchoyo (hapa inakanusha ya kwamba Amina hana uhusiano tabia ya uchoyo).
  • Kikombe ki mezani (hapa kipashio cha ki kimetumika kutaja mazingira au mahali kikombe kilipo - kiko mezani).
  • Juma yu mgonjwa (hapa inataja tena hali ya nafsi - ni mgonjwa).

Angalizo: Kitenzi kishiriki alama yake ni t ndogo.

Aina za vitenzi vishirikishi

Aina za vitenzi vishirikishi vimegawanyika katika makundi makuu mawili - navyo ni:

1) Vitenzi vishirikishi vikamilifu

2) Vitenzi vishiriki vipungufu

Tazama pia

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitenzi kishirikishi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.