Kizizi cha jino
Kizizi cha jino ni sehemu ya jino iliyopo chini ya kichwa cha jino au tajino. Kizizi kinashika jino katika taya.
Kizizi hufunikwa kwa sementi ya jino na kinajengwa kwa dentini ambayo ni aina ya mfupa.
Kwa kawaida vizizi vya jino vinaishia kwenye ncha kali na kuwa na urefu mara mbili kama tajino.
Kwenye ncha ya kizizi (kwa Kilatini apex dentis) kuna tundu (kwa Kilatini Foramen apicale dentis) ambako fofota yaani neva na mishipa ya damu vinaingia ndani ya uwazi wa jino. Kiingilio hiki cha mishipa huitwa pia kanali ya jino.
Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kizizi cha jino kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |