Krispo wa Korintho

Krispo wa Korintho alikuwa Myahudi wa Korintho (Ugiriki) katika karne ya 1.

Matendo ya Mitume (18:8) kinamtaja kati ya wale waliomsikiliza kwa imani Mtume Paulo alipohubiri katika sinagogi la mji huo mwaka 50 hivi. Paulo mwenyewe alimbatiza (1Kor 1:14). Kwa kuwa alikuwa mkuu wa sinagogi hilo, alivuta wengi katika Ukristo, ila ilimbidi aache uongozi. Hata hivyo aliyemrithi, Sosthene, akawa mwanafunzi wa Paulo vilevile.

Inasimuliwa kwamba baadaye akawa askofu wa Kalsedonia (leo nchini Uturuki) na hatimaye aliuawa kwa sababu ya imani yake.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 4 Oktoba.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Krispo wa Korintho kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.