Kristie Lu Stout (amezaliwa 7 Desemba 1974) ni mwandishi wa habari na mtangazaji kutoka Marekani anayefanya kazi CNN International.

Kristie Lu Stout mnamo Januari 2008.

Wasifu

hariri

Stout alisoma katika Shule ya Upili ya Lynbrook mjini San Jose, California, ambako alikuwa mwanachama mwanzilishi wa Lynbrook Speech and Debate Club, na vilevile alikuwa kielelezo bora kati ya vijana wenziwe.[1] Yeye alipata shahada ya kwanza na ya pili katika Uanahabari kutoka Chuo Kikuu cha Stanford, na akasomea Kichina katika Chuo Kikuu cha Tsinghua mjini Beijing. [2]

Ndiye mtangazaji wa kipindi cha CNN Today, kinachoonyeshwa kila siku na kilichomfanya ashinde tuzo kutoka Asia Television Award kama Mtangazaji Bora.[3] Kabla ya hapo, aliwahi kutangaza kwenye kipindi cha CNN kinachohusisha teknolojia kiitwacho Spark, kipande chao cha kila siku "Tech Watch" , na kipindi cha Global Office . Yeye pia alikuwa akiandika "Beijing Byte" kwenye gazeti la South China Morning Post, na alikuwa mhariri wa Wired.com [2] na mwanachama mwanzilishi wa Sohu.

Stout anaishi nchini Hong Kong na aliolewa na wakili Seung Chong.[1]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 "The Frequent Flyers' Friend". Stanford Magazine. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-02-20. Iliwekwa mnamo 2008-08-07.
  2. 2.0 2.1 "A Day in the Life of a Multi-Platform Journalist". ACM Ubiquity. Iliwekwa mnamo 2007-03-01.
  3. "Asian Television Awards 2006 Winners". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-10-16. Iliwekwa mnamo 2007-09-06.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kristie Lu Stout kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.