Kichina
Kichina ni lugha za Wachina nchini China na kote duniani wanapoishi. Ni tawi kubwa la kundi la lugha za Kichina-Kitibet.
Kundi ya lugha na lahaja
haririHali halisi ni zaidi ya lugha moja bali ni kundi ya lugha na lahaja mbalimbali. Wakisema kikwao hawaelewani kati yao lakini tangu miaka 1000 wote walitumia mwandiko mmoja mwenye alama hizihizi. Mwandiko wa Kichina hutumia alama moja kwa neno lote kwa hiyo kila mtu anaelewa mwandiko hata akisoma na kutamka tofauti.
Idadi ya Wasemaji
haririIdadi ya wasemaji wa lugha za Kichina ni takriban 1,200,000,000 au zaidi ya watu bilioni moja. Hadi mwanzo wa karne ya 20 tofauti kati ya lugha na lahaja illikuwa kubwa sana. Tangu mapinduzi ya China ya 1911 aina ya lugha rasmi imejengwa inayoitwa Kimandarini. Siku hizi inajadiliwa au angalau kueleweka kati ya idadi kubwa ya Wachina wote. Bado wasemaji wa lugha zote za Kichina huelewana kupitia mwandiko - kama ni wasomi.
Lugha na lahaja kuu za Kichina
haririWataalamu huhesabu kundi nne za lahaja ndani ya Kichina kwa jumla pamoja na idadi ya wasemaji:
- Guan (Mandarin) 北方話/北方话 or 官話/官话, (mnamo milioni 850),
- Wu 吳/吴 (pamoja na Shanghai) (manmo milioni 90),
- Yue (Cantonese) 粵/粤, (mnamo milioni 80),
- Min 閩/闽, which includes Taiwanese, (mnamo milioni 50),
- Xiang 湘, (mnamo milioni 35),
- Hakka 客家 or 客, (mnamo milioni 35),
- Gan 贛/赣, (mnamo milioni 20)
Mwandiko
haririKichina huandikwa kwa alama zinazomaanisha neno moja si sillabi au herufi tu. Lakini maneno mengi ya Kichina yana silabi moja tu. Kamusi kubwa ya lugha ina alama zaidi ya 40,000- Wachina wasomi wenye elimu nzuri hujua takriban alama 6,000 hadi 7,000. Gazeti la kawaida hutumia alama 3,000. Serikali inasema mtu ajua kuandika na kusoma kama ameshika angalau alama 2,000.
Tangu mapinduzi ya Kichina ya 1949 serikali imesambaza alama zilizorahisishwa. Kuna pia mipango ya kulatinishi lugha yaani kuendeleza namna ya kuandika lugha kwa herufi za Kilatini.
Viungo vya Nje
hariri- makala za OLAC kuhusu Kichina Ilihifadhiwa 11 Agosti 2015 kwenye Wayback Machine.
- lugha ya Kichina katika Glottolog
- http://www.ethnologue.com/language/cmn
- I Love Chinese Learning Chinese Magazine
- Learn Chinese Ilihifadhiwa 19 Septemba 2021 kwenye Wayback Machine. Free Chinese Learning Lessons and mp3
- Free Chinese Character Input Software Ilihifadhiwa 7 Mei 2008 kwenye Wayback Machine. Google Pinyin Input Software
- Chinese Pinyin Ilihifadhiwa 1 Septemba 2021 kwenye Wayback Machine. a brief introduction to standard Chinese phonetic system
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kichina kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |