Kumbikumbi ni mchwa wenye mabawa wanaotoka katika kichuguu wakati wa majira ya mvua. Mchwa hao ni majike na madume waliokomaa na wakiruka wanapandana. Kwa sababu kumbikumbi wa vichuguu vingi vya mahali pamoja hutoka kwa wakati mmoja wanaweza kuchagua mwenzi kutoka kichuguu kisicho chao. Halafu kila jozi inachimba kishimo na kuzaa na kuanza kichuguu kipya.

Kumbikumbi wakiruka baada ya mvua

Lakini asilimia ndogo tu ya kumbikumbi huishi hadi kuzaa. Wengi sana huliwa na mbuai kama vile ndege, popo, nguchiro n.k. Hata watu huwala kwa sababu kumbikumbi wana mafuta mengi ndani ya miili yao.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kumbikumbi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.