Mchwa
Mchwa wafanya kazi na askari
Mchwa wafanya kazi na askari
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Blattodea
Oda ya chini: Isoptera (Wadudu ambao mabawa yao yote ni sawa)
Brullé, 1832
Ngazi za chini

Familia 10:

  • †Archeorhinotermitidae Krishna & Grimaldi, 2003
  • Archotermopsidae Engel, Grimaldi & Krishna, 2009
  • †Cratomastotermitidae Bechly, 2007
  • Hodotermitidae Desneux, 1904
  • Kalotermitidae Enderlein, 1909
  • Mastotermitidae Desneux, 1904
  • Rhinotermitidae Froggat, 1897
  • Serritermitidae Holmgren, 1910
  • Stolotermitidae Homgren, 1910
  • Stylotermitidae K. Holmgren & N. Holmgren, 1917
  • Termitidae Latreille, 1802
  • Termopsidae Holmgren, 1911

Mchwa ni wadudu wadogo wa oda ya chini Isoptera katika oda Blattodea wanaoishi kwa makoloni makubwa katika vichuguu. Kuna aina ya mchwa ambao huishi ndani ya mbao au miti. Takriban spishi zote hula ubao.

Kila koloni lina malkia, mfalme, askari na wafanyakazi. Askari na wafanyakazi hawana mabawa lakini malkia na mfalme waliwahi kuwa na mabawa walipokuwa vijana. Mfalme anamtia malkia mbegu na huyu anazaa mayai mengi sana. Askari wanalinda kichuguu na wafanyakazi wanafanya kazi nyingine zote.

Mara kwa mara wafanyakazi wanawapatia majana kadhaa chakula fulani ili wawe wadudu wanaoweza kuzaa. Wadudu hawa wana mabawa na huitwa kumbikumbi.[1]

Utafiti wa hivi karibuni waonyesha mchwa, hasa mchwa wa Jangwa la Sahara, kuwa ndiye mnyama anayestahimili joto zaidi. Spishi hii ya mchwa inaweza kustahimili joto hadi nyuzi 55.1.[2]

Bidii na umoja

Mdudu huyu huishi kwa kushirikiana na kutangamana. Yeye halali kabla hajatafuta chakula cha kutosha na cha kuweka akiba.

Hivyo mchwa wametumika katika hadithi nyingi za kitoto ili kufunza maadili ya bidii na umoja. Kwa kawaida, mchwa hukaa wote pamoja katika koloni.

Mwandishi Aesop pia aliandika kuhusu bidii ya mchwa katika hadithi yake 'The Ant and the Grasshopper'.

Katika maandiko ya Biblia (kitabu cha Methali), waumini wameombwa waige mchwa katika utendakazi na umoja.

Katika kitabu kitakatifu cha Waislamu cha Kurani, Sulemani alisikia mchwa akiwaonya wengine warudi nyumbani wasije wakapondwapondwa.

Usumbufu wa mchwa

Hata hivyo, watu wengi huona mchwa kama wasumbufu, haswa anapoishi karibu na majengo ya watu. Mchwa hula mbao na kwa hiyo huharibu milango, samani na maboriti ya nyumba.

Wale wanaoishi ndani ya mbao na kula vifaa vya mbao nyumbani huleta pia tatizo la uchafu kutokana na kinyesi chao.[3] Kwa hiyo, watu wengi hutafuta dawa za kuua wadudu hawa au njia nyingine asili za kuwadhibiti kama vile utumizi wa udongo Diatomaceous au mafuta ya kitunguu saumu zinazoathiri wadudu[4].

Wanaofanya taaluma hiyo kwanza huangalia mchwa ni wa aina gani ili waweze kujua amejificha wapi maana wao hujifinya pahala kwingi.

Spishi kadhaa za Afrika

Picha

Tanbihi

  1. Termite Larvae – What Does Baby Termite Look Like? (en-US). PestsGuide (2018-11-24). Iliwekwa mnamo 2019-02-13.
  2. Nic Fleming. The ant that is the hottest insect in the world (en). www.bbc.com. Iliwekwa mnamo 2019-02-13.
  3. Kuhusu kinyesi cha mchwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-04-07. Iliwekwa mnamo 2019-04-07. Archived 7 Aprili 2019 at the Wayback Machine.
  4. Ambru (2018-11-24). How to Get Rid of Termites: A Comprehensive Guide (2019) (en-US). PestsGuide. Iliwekwa mnamo 2019-06-17.

Marejeo

  Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mchwa kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.