Kutengwa kwa Vijana
Kutengwa kwa Vijana ni aina ya kutengwa kwa jamii ambayo vijana wako katika changamoto ya kijamii katika kujiunga na taasisi na mashirika katika jamii zao. Uchumi wenye matatizo, upungufu wa programu za kiserikali, na vikwazo vya kielimu ni mifano ya matatizo katika taasisi za kijamii ambayo yanachangia kutengwa kwa vijana kwa kufanya iwe vigumu zaidi kwa vijana kubadilika kuwa watu wazima. Serikali za Ulaya hivi karibuni zimetambua mapungufu haya katika miundo ya mashirika ya jamii na zimeanza kuchunguza upya sera kuhusu kutengwa kwa jamii.[1] Sera nyingi zinazoshughulikia kutengwa kwa jamii zinawalengwa vijana kwaidadi kubwa inayokabiliwa na mabadiliko ya watu wazima.
Kutengwa kwa vijana kuna pande nyingi katika umri, rangi, jinsia, tabaka na mtindo wa maisha yote huathiri uzoefu wa maisha ya vijana ndani ya utamaduni fulani. Huu mwingiliano huathiri kiwango ambacho kijana mmoja mmoja huisi kutengwa. Vile vile, kutengwa kwa vijana ni kawaida kwa muktadha. Hii ina maana kwamba vijana wametengwa na jamii kwa njia tofauti kulingana na maeneo yao ya kitamaduni na mazingira. Tofauti rahisi kati ya fursa na rasilimali zinazotolewa katika mtaa mmoja inaweza kuleta mgawanyiko kati ya vijana ambao wamejumuishwa na vijana ambao wametengwa na jamii zao. Jambo lingine la kuzingatia ni kwamba kutengwa kwa vijana ni kimahusiano kwa vile kutengwa kwa jamii kuna pande mbili, waliotengwa na waliotenga.
Chanzo cha kutengwa kwa vijana
haririKutengwa kwa vijana kunaweza kuchunguzwa kwa kugawa sababu zake katika mambo ya kijamii na kitamaduni. Kimuundo sababu za kutengwa ni pamoja na ukosefu wa usawa katika Mamlaka za kisiasa. Ukosefu wa ajira wa muda mrefu na mapato ya chini yanaweza kuathiri uwezo wa mtu wa kufikia miundo ya kijamii ambayo huendeleza mtu katika jamii kwa kufungua milango ya fursa mpya na kujenga hisia ya kukubalika na ushirikishwaji wa jamii.[2]
Umaskini
haririUmaskini ni chanzo mojawapo cha kutengwa kwa vijana.[3] Umaskini ni hali ya kujitenga inayoathiri miunganisho ya kijamii ya watu na uwezo wa kuchangia katika shughuli mahususi za kitamaduni zinazojenga jamii. Kama mwanasosholojia Peter Townshend anavyoeleza; "Watu binafsi, familia na vikundi vinaweza kusemwa kuwa katika umaskini, wakati rasilimali zao ziko chini sana zile zinazoamriwa na mtu wa kawaida au familia kiasi kwamba, kwa kweli, wametengwa na mifumo ya maisha ya kawaida, mila na desturi"[4]
Kutengwa kwa vijana kikanda
haririKwa kuzingatia kwamba ufafanuzi wa kutengwa kwa vijana hutofautiana katika tamaduni, dhana hii lazima ijumuishe uchambuzi wa maana ya kuwa mwanachama wa jamii fulani, kwa mfano, "uchambuzi wa maana ya kuwa Misri, Morocco, Irani, au Syria, kuwa Muislamu, Mwarabu, na kadhalika.” [5] Ndani ya nchi, vitongoji au majimbo yanaweza kugawanywa kwa njia ambayo hata vijana tofauti katika utamaduni wanaweza kutengwa katika viwango tofauti. [6] Utandawazi huleta ubaguzi linganishi katika jamii. "Utandawazi umetoa mgawanyiko wa wafanyakazi katika sura mpya ya kimataifa, ambayo inapendelea sana mataifa ya Magharibi kuliko Afrika. [7] Kwa hivyo, vijana wanaoingia katika soko la ajira katika Ukanda wa Kusini mwa Dunia wanaathiriwa na vitendo vya nchi za Kaskazini mwa Dunia.
Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini (MENA)
haririMashariki ya Kati na Afrika Kaskazini ( MENA ), kutengwa kwa vijana kunatofautiana kwa namna mbalimbali. Kama ilivyo katika mikoa mingine, ukosefu wa ajira kwa vijana ni mkubwa, na wastani wa kikanda kwa 25% ukosefu wa ajira kati ya umri wa miaka 15 hadi 24, [8] ambao unafikia juu kama 37% nchini Morocco na hadi 73% nchini Syria . [9] Pia kuna viwango vikubwa vya mgawanyiko wa soko la ajira kuhusiana na urekebishaji wa uchumi na masuala ya ndani na nje.
Marejeo
hariri- ↑ Ambrosio, Conchita D. and Carlos Gradín. 2003. "Income Distribution and Social Exclusion of Children: Evidence from Italy and Spain in the 1990s*." Journal of Comparative Family Studies 34(3):479-XII
- ↑ Hunter, Boyd and Kirrily Jordan. 2010. "Explaining Social Exclusion: Towards Social Inclusion for Indigenous Australians." Australian Journal of Social Issues 45(2):243-265,153
- ↑ Concannon, Liam (2008). "Citizenship, sexual identity and social exclusion". International Journal of Sociology and Social Policy. 28 (9/10): 326–339. doi:10.1108/01443330810900176.
- ↑ Levitas, R. (2006) "The concept and measurement of social exclusion" Archived Machi 4, 2016, at the Wayback Machine, In C. Pantazis, D. Gordon and R. Levitas (eds.) Poverty and Social Exclusion in Britain: The Millennium Survey, Bristol, Policy Press.
- ↑ Silver, Hilary (2007). "Social Exclusion: Comparative Analysis of Europe and Middle East Youth". Middle East Youth Initiative Working Paper No. 1: 5–6. SSRN 1087432.
- ↑ Ruck, Martin D.; Park, Henry; Killen, Melanie; Crystal, David S. (2011). "Intergroup Contact and Evaluations of Race-Based Exclusion in Urban Minority Children and Adolescents". Journal of Youth and Adolescence. 40 (6): 633–643. doi:10.1007/s10964-010-9600-z. PMC 4090110. PMID 21052799.
- ↑ Makwemoisa, Anthonia (2002). "Youth Existence and the Conditions of Exclusion and Underdevelopment in Nigeria". Journal of Cultural Studies. 4. doi:10.4314/jcs.v4i1.6190.
- ↑ Navtej Dhillon & Tarik Yousef, “Inclusion: Meeting the 100 Million Youth Challenge,” Ilihifadhiwa 10 Machi 2014 kwenye Wayback Machine. Middle East Youth Initiative, 2007
- ↑ Silver, Hilary (2007). "Social Exclusion: Comparative Analysis of Europe and Middle East Youth". Middle East Youth Initiative Working Paper No. 1: 5–6. SSRN 1087432.