Kuzaa kwa upasuaji

Kuzaa kwa upasuaji ni namna ya kujifungua watoto kwa njia ya upasuaji.[2] Kuzaa kwa upasuaji mara nyingi ni muhimu wakati kuzaa kupitia uke kunaweza kumweka mtoto au mama katika hatari.[2] Sababu zinaweza kujumuisha leba iliyozuiliwa, mimba ya mapacha, shinikizo la damu kwa mama, kuzaa kwa kutanguliza miguu ya mtoto, au matatizo ya kondo la nyuma au kiunga mwana.[2][3] Kuzaa kwa upasuaji kunaweza kufanywa kulingana na umbo la pelvisi ya mama au historia ya kuzaa kwa upasuaji kulikotangulia.[2][3] Kujaribu kuzaa kupitia uke baada ya kupasuliwa kunawezekana.[2] Shirika la Afya Duniani linapendekeza kwamba kuzaa kwa kupasuliwa kufanyike ikiwa hilo ni lazima kiafya.[3][4] Baadhi ya kuzaa kwa upasuaji hufanywa bila sababu za kimatibabu, bali kwa ombi la mtu, hasa mama mwenyewe.[2]

Kundi la madaktari likizalisha kwa njia ya upasuaji wa Kikaizari.[1]

Kuzaa kwa upasuaji kwa kawaida huchukua dakika 45 hadi saa moja.[2] Njia hii inaweza kufanywa kwa kizuizi cha mgongo (sindano ya uti wa mgongo inayozuia uchungu), ambapo mwanamke huwa macho, au chini ya kitia ganzi cha jumla.[2] Katheta (mrija) ya mkojo hutumiwa kuondoa mkojo katika kibofu, kisha ngozi ya tumbo husafishwa kwa dawa ya kuua viini.[2] Kisha kwa kawaida chale ya takriban sentimita 15 (inchi 6) hupitishwa kwenye fumbatio la chini la mama.[2] Kisha uterasi hufunguliwa kwa chale ya pili na mtoto kuzaliwa.[2] Kisha chale hizo hushonwa na kufungwa.[2] Kwa kawaida, mwanamke anaweza kuanza kunyonyesha mara tu anapotoka kwenye chumba cha upasuaji na kuwa macho.[5] Mara nyingi, mwanamke anahitajika kuwa hospitalini kwa siku kadhaa kabla ya kupona na kurudi nyumbani.[2]

Kuzaa kwa kupasuliwa kwa husababisha ongezeko dogo la jumla la matokeo duni katika mimba zenye hatari ndogo.[3] Pia kwa kawaida huchukua muda mrefu kupona, kama vile wiki sita, kuliko kuzalia kwenye uke.[2] Hatari zilizoongezeka ni pamoja na matatizo ya kupumua kwa mtoto na kuingia kwa maji ya amnioni kwenye mzunguko wa damu ya mama na kutokwa na damu baada ya kuzaa kwa mama.[3] Miongozo iliyowekwa inapendekeza kwamba kuzaa kwa upasuaji kusitumike kabla ya wiki 39 za ujauzito bila sababu ya kimatibabu.[6] Mbinu hii ya kujifungua haionekani kuathiri utendaji wa ngono unaofuata.[7]

Mnamo mwaka wa 2012, kuzaa kwa upasuaji karibu milioni 23 kulifanywa ulimwenguni.[8] Jumuiya ya kimataifa ya huduma za afya hapo awali imezingatia kiwango cha 10% na 15% kuwa bora cha kuzaa kwa upasuaji.[4] Ushahidi fulani umepata kwamba kiwango cha juu cha 19% kinaweza kusababisha matokeo bora.[8] Zaidi ya nchi 45 duniani zina viwango vya kuzaa kwa upasuaji vya chini ya 7.5%, wakati zaidi ya 50 zina viwango vya zaidi ya 27%.[8] Juhudi zinafanywa ili kuboresha ufikiaji na kupunguza matumizi ya kuzaa kwa upasuaji.[8] Nchini Marekani, kufikia mwaka wa 2017, takriban 32% ya waliojifungua walikuwa kwa njia ya kuzaa kwa upasuaji.[9] Upasuaji huo umefanywa tangu angalau miaka 715 Kabla ya Kristo kufuatia kifo cha mama, huku mtoto akinusurika mara kwa mara.[10] Maelezo ya akina mama walionusurika yalianza miaka ya 1500.[10] Kwa kuanzishwa kwa dawa za kuua viini na vitia ganzi katika karne ya 19, kuokolewa kwa maisha ya mama na mtoto kumekuwa kwa kawaida.[10]

Marejeo

hariri
  1. Fadhley, Salim (2014). "Caesarean section photography". WikiJournal of Medicine. 1 (2). doi:10.15347/wjm/2014.006.
  2. 2.00 2.01 2.02 2.03 2.04 2.05 2.06 2.07 2.08 2.09 2.10 2.11 2.12 2.13 "Pregnancy Labor and Birth". Office on Women’s Health, U.S. Department of Health and Human Services. 1 Februari 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Julai 2017. Iliwekwa mnamo 15 Julai 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 "Safe Prevention of the Primary Cesarean Delivery". American Congress of Obstetricians and Gynecologists and the Society for Maternal-Fetal Medicine. Machi 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Machi 2014. Iliwekwa mnamo 20 Februari 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 "WHO Statement on Caesarean Section Rates" (PDF). 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 1 Mei 2015. Iliwekwa mnamo 6 Mei 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Lauwers, Judith; Swisher, Anna (2010). Counseling the Nursing Mother: A Lactation Consultant's Guide (kwa Kiingereza). Jones & Bartlett Publishers. uk. 274. ISBN 9781449619480. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Septemba 2017.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. American Congress of Obstetricians and Gynecologists, "Five Things Physicians and Patients Should Question", Choosing Wisely: an initiative of the ABIM Foundation, American Congress of Obstetricians and Gynecologists, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Septemba 2013, iliwekwa mnamo 1 Agosti 2013{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Yeniel, AO; Petri, E (Januari 2014). "Pregnancy, childbirth, and sexual function: perceptions and facts". International Urogynecology Journal. 25 (1): 5–14. doi:10.1007/s00192-013-2118-7. PMID 23812577.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. 8.0 8.1 8.2 8.3 Molina, G; Weiser, TG; Lipsitz, SR; Esquivel, MM; Uribe-Leitz, T; Azad, T; Shah, N; Semrau, K; Berry, WR (1 Desemba 2015). "Relationship Between Cesarean Delivery Rate and Maternal and Neonatal Mortality". JAMA. 314 (21): 2263–70. doi:10.1001/jama.2015.15553. PMID 26624825.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "Births: Provisional Data for 2017" (PDF). CDC. Mei 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 17 Mei 2018. Iliwekwa mnamo 18 Mei 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. 10.0 10.1 10.2 Moore, Michele C.; Costa, Caroline M. de (2004). Cesarean Section: Understanding and Celebrating Your Baby's Birth (kwa Kiingereza). JHU Press. uk. Chapter 2. ISBN 9780801881336. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Julai 2020. Iliwekwa mnamo 29 Julai 2020.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)