Kujifungua
Kujifungua ni mwisho wa ujauzito ambapo mtoto mmoja au zaidi hutoka kwenye tumbo la uzazi kwa kupitia uke au kwa upasuaji.[1]
Mnamo mwaka wa 2015, walizaliwa watoto wapatao milioni 135 ulimwenguni.[2] Takriban milioni 15 walizaliwa kabla ya wiki 37 za ujauzito,[3] huku kati ya asilimia 3 na 12 walizaliwa baada ya wiki 42.[4] Katika ulimwengu ulioendelea, kuzaa kwingi hutokea hospitalini,[5] [6] wakati katika ulimwengu unaoendelea kuzaa kwingi hufanyika nyumbani kwa usaidizi wa mkunga. [7]
Njia ya kawaida ni kuzaa kupitia uke.[8] Inahusisha hatua tatu za kuzaa: kufupisha na kufunguka kwa seviksi, kushuka na kuzaliwa kwa mtoto, na utoaji wa kondo la nyuma.[9] Hatua ya kwanza kwa kawaida huchukua saa 12 hadi 19, hatua ya pili dakika 20 hadi saa mbili, na hatua ya tatu dakika tano hadi 30.[10] Hatua ya kwanza huanza na maumivu makali ya tumbo au mgongo ambayo hudumu karibu nusu dakika na kutokea kila dakika 10 hadi 30. Maumivu haya huwa na nguvu na kutokea karibu karibu kwa pamoja kwa muda.[10] Wakati wa hatua ya pili, kusukuma kwa mikazo kunaweza kutokea.[10] Katika hatua ya tatu, kuchelewesha kushikilia kitovu kwa ujumla kunapendekezwa.[11] Mbinu kadhaa zinaweza kusaidia kwa maumivu, kama vile mbinu za kutuliza, afyuni, na kutiwa ganzi migongoni.[10]
Watoto wengi huzaliwa kuwa kutoa kichwa kwanza; hata hivyo takriban 4% huzaliwa kwa kutoa miguu au matako kwanza, inayojulikana kama chini kwanza badala ya kichwa kwanza.[10] [12] Kwa kawaida, kichwa huingia kwenye pelvisi ikitazama upande mmoja, na kisha huzunguka kuelekea chini. Wakati wa leba, mwanamke anaweza kwa ujumla kula na kuzunguka apendavyo.[13] Hata hivyo, kusukuma haipendekezi wakati wa hatua ya kwanza au wakati wa kujifungua kwa kichwa, na kuingiza kioevu kwenye tupu ya nyuma hakupendekezwi.[13] Wakati kukata sehemu iliyo wazi kwenye uke, inayojulikana kama kukata sehemu ya kati ya uke na tupu ya nyuma kwa ujumla hakuhitajiki.[10] Mnamo mwaka wa 2012, karibu milioni 23 walijifungua kupitia upasuaji wa sehemu ya kati ya tumbo na uterasi.[14] Upasuaji wa sehemu ya kati ya tumbo na uterasi unaweza kupendekezwa kwa mapacha, dalili za kufadhaika kwa mtoto, au ikiwa mtoto atatoa kwa miguu kabla ya kichwa.[10] Njia hii ya kujifungua inaweza kuchukua muda mrefu kupona.[10] Dozi moja ya antibiotiki, azithromycin, inaweza kutumika kuzuia maambukizi katika nchi za kipato cha chini na cha kati.[15]
Kila mwaka, matatizo kutokana na ujauzito na kuzaa husababisha vifo vya wajawazito 500,000, wanawake milioni saba wana matatizo makubwa ya muda mrefu, na wanawake milioni 50 wana matokeo mabaya ya afya baada ya kujifungua.[16] Mengi ya haya hutokea katika nchi zinazoendelea.[16] Matatizo mahususi ni pamoja na leba iliyozuiliwa, kuvuja damu baada ya kuzaa, kuzimia wakati wa ujauzito au muda mfupi baada ya kujifungua, na maambukizi ya baada ya kujifungua.[16]
Matatizo kwa mtoto yanaweza kujumuisha ukosefu wa oksijeni wakati wa kuzaliwa, kiwewe cha kuzaliwa, kuzaliwa kabla ya wakati, na maambukizo.[17][18]
Marejeo
hariri- ↑ Martin, Elizabeth (2015). Concise Colour Medical l.p.Dictionary (kwa Kiingereza). Oxford University Press. uk. 375. ISBN 978-0-19-968799-2. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-11.
- ↑ "The World Factbook". www.cia.gov. Julai 11, 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Novemba 2016. Iliwekwa mnamo 30 Julai 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Preterm birth Fact sheet N°363". WHO. Novemba 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Machi 2015. Iliwekwa mnamo 30 Julai 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Buck, Germaine M.; Platt, Robert W. (2011). Reproductive and perinatal epidemiology. Oxford: Oxford University Press. uk. 163. ISBN 978-0-19-985774-6. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-11.
- ↑ Co-Operation, Organisation for Economic; Development (2009). Doing better for children. Paris: OECD. uk. 105. ISBN 978-92-64-05934-4. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-11.
- ↑ Olsen O, Clausen JA (Septemba 2012). "Planned hospital birth versus planned home birth". The Cochrane Database of Systematic Reviews (9): CD000352. doi:10.1002/14651858.CD000352.pub2. PMC 4238062. PMID 22972043.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Fossard, Esta de; Bailey, Michael (2016). Communication for Behavior Change: Volume lll: Using Entertainment–Education for Distance Education. SAGE Publications India. ISBN 978-93-5150-758-1. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Septemba 2017. Iliwekwa mnamo 31 Julai 2016.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Memon HU, Handa VL (Mei 2013). "Vaginal childbirth and pelvic floor disorders". Women's Health. 9 (3): 265–77, quiz 276–77. doi:10.2217/whe.13.17. PMC 3877300. PMID 23638782.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Birth". The Columbia Electronic Encyclopedia (6 ed.). Columbia University Press. 2016. http://www.encyclopedia.com/topic/birth.aspx#5. Retrieved 2016-07-30.
- ↑ 10.0 10.1 10.2 10.3 10.4 10.5 10.6 10.7 "Pregnancy Labor and Birth". Women's Health. Septemba 27, 2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Julai 2016. Iliwekwa mnamo 31 Julai 2016.
The first stage begins with the onset of labor and ends when the cervix is fully opened. It is the longest stage of labor, usually lasting about 12 to 19 hours
..
The second stage involves pushing and delivery of your baby. It usually lasts 20 minutes to two hours.{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ McDonald SJ, Middleton P, Dowswell T, Morris PS (Julai 2013). "Effect of timing of umbilical cord clamping of term infants on maternal and neonatal outcomes". The Cochrane Database of Systematic Reviews. 7 (7): CD004074. doi:10.1002/14651858.CD004074.pub3. PMC 6544813. PMID 23843134.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Hofmeyr GJ, Hannah M, Lawrie TA (Julai 2015). "Planned caesarean section for term breech delivery". The Cochrane Database of Systematic Reviews (7): CD000166. doi:10.1002/14651858.CD000166.pub2. PMC 6505736. PMID 26196961.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 13.0 13.1 Childbirth: Labour, Delivery and Immediate Postpartum Care (kwa Kiingereza). World Health Organization. 2015. uk. Chapter D. ISBN 978-92-4-154935-6. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Septemba 2017. Iliwekwa mnamo 31 Julai 2016.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Molina G, Weiser TG, Lipsitz SR, Esquivel MM, Uribe-Leitz T, Azad T, Shah N, Semrau K, Berry WR, Gawande AA, Haynes AB (Desemba 2015). "Relationship Between Cesarean Delivery Rate and Maternal and Neonatal Mortality". JAMA. 314 (21): 2263–70. doi:10.1001/jama.2015.15553. PMID 26624825.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Tita, Alan T.N.; Carlo, Waldemar A.; McClure, Elizabeth M.; Mwenechanya, Musaku; Chomba, Elwyn; Hemingway-Foday, Jennifer J.; Kavi, Avinash; Metgud, Mrityunjay C.; Goudar, Shivaprasad S. (30 Machi 2023). "Azithromycin to Prevent Sepsis or Death in Women Planning a Vaginal Birth". New England Journal of Medicine. 388 (13): 1161–1170. doi:10.1056/NEJMoa2212111.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 16.0 16.1 16.2 Education material for teachers of midwifery : midwifery education modules (PDF) (tol. la 2nd). Geneva [Switzerland]: World Health Organisation. 2008. uk. 3. ISBN 978-92-4-154666-9. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2015-02-21.
- ↑ Martin, Richard J.; Fanaroff, Avroy A.; Walsh, Michele C. (2014-08-20). Fanaroff and Martin's Neonatal-Perinatal Medicine: Diseases of the Fetus and Infant (kwa Kiingereza). Elsevier Health Sciences. uk. 116. ISBN 978-0-323-29537-6. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-11.
- ↑ World Health Organization. "Newborns: reducing mortality". World Health Organization. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Aprili 2017. Iliwekwa mnamo 1 Februari 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)