Pimbi
(Elekezwa kutoka Kwanga)
Pimbi | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Pimbi mkubwa kwenye Mlima Kenya (Procavia capensis)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Jenasi 3, spishi 4:
|
Pimbi, kwanga, perere au wibari ni wanyama wadogo wa familia Procaviidae. Jina la kwanga litumika kwa jenasi Heterohyrax na perere na wibari yatumika kwa jenasi Dendrohyrax. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara na Mashariki ya Kati, mara nyingi katika maeneo makavu na yenye miamba mingi. Spishi zote ni nene zenye mkia mfupi na manyoya mazito. Miguu yao ina vitakia vyenye ngozi nene na tezi nyingi za jasho ambavyo vinawasaidia kupanda miamba na miti. Rangi yao ni kijivu, kahawia au hudhurungi. Hula majani ya manyasi, ya mimea na ya miti.
Spishi
hariri- Dendrohyrax arboreus, Wibari au Perere Kusi (Southern Tree Hyrax au Tree Dassie)
- Dendrohyrax dorsalis, Wibari au Perere Magharibi (Western Tree Hyrax au Tree Dassie)
- Heterohyrax brucei, Kwanga au Pimbi Mdogo (Yellow-spotted Rock Hyrax au Bush Hyrax)
- Procavia capensis, Pimbi Mkubwa (Rock Hyrax au Cape Hyrax)
Picha
hariri-
Perere kusi
-
Perere magharibi
-
Kwanga
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.