Lango:Jiografia/Intro
Jiografia ni somo la Dunia na vipengele vyake, wakazi wake, na maajabu yake. Neno jiografia linatokana na maneno ya Kigiriki gê ("Dunia") na graphein ("kuandika"). Ina maana ya "kuandika kuhusu Dunia". Neno hili lilianza kutumiwa na mwanasayansi Eratosthenes (276-194 KK).
Sehemu za jiografia ni vitu kama mabara, bahari, mito na milima. Wakazi wake ni watu wote na wanyama waishio juu yake. Maajabu yake ni vitu vinavyotokea, kama vile maji kujaa na kupwa, upepo, na tetemeko la ardhi.