Lemuri-mwanzi
Lemuri-mwanzi | ||||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Lemuri-mwanzi mkubwa
| ||||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||||
|
Lemuri-mwanzi (kutoka Kiingereza: bamboo lemur) ni spishi za lemuri wa jenasi Hapalemur na Prolemur katika familia Lemuridae. Kama lemuri wote wanatokea Madagaska tu. Wana manyoya kijivu hadi kahawia. Urefu wa mwili ni sm 26-46 na mkia una urefu sawa au mrefu zaidi. Lemuri-mwanzi mkubwa ni sm 40-50 na ana uzito wa kg 2-2.5. Hula machipukizi, majani na gale za miwani hasa, na pengine nyoga, maua na matunda.
Spishi
hariri- Hapalemur alaotrensis, Lemuri-mwanzi wa Alaotra (Lac Alaotra gentle lemur)
- Hapalemur aureus, Lemuri-mwanzi Dhahabu (Golden bamboo lemur)
- Hapalemur gilberti, Lemuri-mwanzi wa Gilbert (Gilbert's bamboo lemur)
- Hapalemur griseus, Lemuri-mwanzi Mdogo Mashariki Eastern lesser bamboo lemur)
- Hapalemur meridionalis, Lemuri-mwanzi Mdogo Kusi (Southern lesser bamboo lemur)
- Hapalemur occidentalis, Lemuri-mwanzi Mdogo Magharibi (Western lesser bamboo lemur)
- Prolemur simus, Lemuri-mwanzi Mkubwa (Greater bamboo lemur)
Picha
hariri-
Lemuri-mwanzi wa Alaotra
-
Lemuri-mwanzi dhahabu
-
Lemuri-mwanzi mdogo mashariki
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.