Lionel Isaac Abrahams (11 Aprili 1928 - 31 Mei 2004) alikuwa mwandishi wa Afrika Kusini. Mwaka wa 1957 alianzisha jarida la fasihi lililoitwa The Purple Renoster [1]. Hasa, Abrahams aliandika hadithi fupi na mashairi. Katika riwaya yake The Celibacy of Felix Greenspan, Abrahams alieleza kitawasifu shida za Myahudi, tena aliyepatwa na ugonjwa wa kupooza, katika maisha ya kila siku nchini Afrika Kusini.[2]

Lionel Abrahams
Amezaliwa 11 Aprili 1928
Pretoria, Afrika Kusini
Amekufa 31 Mei 2004
Nchi Afrika Kusini
Kazi yake Mshairi

Matendo ya Maisha ya Kikazi [3]

hariri

Abrahams alifanya kazi ya karani katika kampuni ya babake kuanzia mwaka wa 1950 hadi 1953. Baada ya kuanzisha The Purple Renoster, alilifanyia kazi jarida hilo kama mwandishi na mhariri wake kuanzia 1957 hadi 1972. Halafu alianzisha makampuni mawili ya uchapishaji na kufanya kazi kama mchapishaji: Renoster Books 1970-1974, na Bateleur Press 1974-1981. Kuanzia 1981 hadi 1992 alikuwa mchapishaji wa jarida la Sesame. Pia kuanzia 1976 hadi 2002 alikuwa mwalimu wa uandishaji.

Maandishi yake

hariri
  • The Celibacy of Felix Greenspan (riwaya, 1976)
  • Journal of a New Man (mashairi, 1984)
  • The Writer in Sand (mashairi, 1988)
  • A Dead Tree Full of Live Birds (mashairi, 1994)

Angalia pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. Ukurasa 481 wa Chapman, Michael. 2003. Southern African Literatures, University of Natal Press. ISBN 1-86914-028-1
  2. Ilan Stavans. "Celibate in Johannesburg." Forward. Forward Pub. Co. 1994. Imeangaliwa tarehe 15 Aprili 2012 kupitia HighBeam Research Archived 9 Aprili 2016 at the Wayback Machine. (lazima kusajiliwa).
  3. Makala ya "Abrahams, Lionel (Isaac)" katika Writers Directory 2005. Imeangaliwa tarehe 15 Aprili 2012 kupitia HighbeamResearch Archived 31 Machi 2002 at the Wayback Machine. (lazima kusajiliwa).
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lionel Abrahams kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.