Lister Elia ni mwanamuziki, mtunzi wa vitabu, mwalimu wa muziki na mkufunzi wa kituo cha mazoezi kutoka Tanzania, lakini kwa sasa anaishi nchini Japani[1][2] Elia alilelewa katika familia ya watu wa dini sana, baba yake akiwa kasisi wa Kanisa la Anglikana la Tanzania, Jimbo la Kati. Alikuwa mpenzi mkubwa wa muziki na alianza kupiga piano akiwa na umri wa miaka sita. Alihitimu elimu ya muziki kutoka Chuo cha Muziki Ruhija kilichopo Bukoba, Tanzania, kisha akaenda kusoma katika chuo kingine kilichopo mjini Wiesen, nchini Austria. Baada ya kuhamia nchini Japani, alijiandikisha katika chuo kingine cha muziki nchini humo kilichojulikana kama MATE School of Music ili kujiendeleza kimuziki zaidi..

Lister Elia
Lister Elia mnamo 2012.
Taarifa za awali
Jina la kuzaliwaLister Elia
AmezaliwaDodoma, Tanzania
Kazi yakeMpiga piano, kinanda, mwalimu, mtunzi wa vitabu, mwanamitindo, mwanafashoni, na mkufunzi wa kituo cha mazoezi cha serikali ya Japani
AlaPiano/kinanda, tarumbeta, gitaa na zumari
Miaka ya kazi1985–present
Ameshirikiana naOrchestra King Kikii Double O, Benebene Group (kiongozi wa bendi), Orchestra Sambulumaa Band, Orchestra Safari Sound, The MK Group
WavutiOfficial website

Elia alijiunga na bendi ya Orchestra King Kikii Double O, ambayo ilikuwa inamilikiwa na Maestro King Kiki. Baadaye akajiunga na kuwa kiongozi wa bendi ya Benebene Group. Bendi yake ya tatu ilikuwa Orchestra Sambulumaa Band, halafu Orchestra Safari Sound (Ndekule), na mwisho kabisa kwa bendi za Tanzania, ni MK Group, kwa kupiga kinanda kwenye wimbo wa "Maumivu Makali".[3] Mwaka mmoja aliyokaa na bendi ya Sambulumaa alirekodi nyimbo zote za albamu ya kwanza ya bendi, aliondoka katika bendi na kujiunga na Orchestra Safari Sound mnamo 1988. Uhamisho huu ulisimamiwa na Abel Baltazar, hasa kazi yake kubwa ilikuwa kukusanya watu na kuwatia kundini na alikuwa mmoja kati ya viongozi wa Orchestra Safari Sounds. Lister Elia vilevile aliwahi kuishi na kufanya kazi muda mchache jijini Nairobi, Kenya, kabala ya kuhamia mazima nchini Japani.

Nchini Nairobi, Elia alipiga piano katika hoteli mbalimbali ikiwa ni pamoja na Jacaranda Hotel, Cassino- Galileo Hall na Tuna Tree Restaurant, Lessa Lassan’s Popolipo na Tchiakatumba. Huko Japani ameungana na rafiki yake wa utotoni maarufu kama Fresh Jumbe, vilevile mwanachama mwenzake wakati yupo Orchestra Safari Sound. Wawili hawa wameunda kundi maarufu kama “The Tanzanites Band-Tokyo. Kazi maarufu ya Lister kwenye kinanda ni pamoja na "Maumivu Makali" na "Mapenzi ya Adhabu" ya MK Group, "Kadiri Mke Wangu" ya Orchestra Sambulumaa,[4], Mayombo ya "Orchestra Sambulumaa""[5], na "Mama Happy" (wimbo maarufu), ambao pia alitunga wakati yupo Sambulumaa[6][7]. Mbali na kazi yake ya muziki, Elia vilevile ni mwalimu wa muziki na mtunzi wa vitabu na hadi sasa keshachapisha vitabu vitabu ikiwa ni pamoja na : The Mystery of Tamko's Death, Jifunze Gitaa na Piano.[8]

Marejeo

hariri
  1. "Once a Teacher,Always a Teacher. LISTER ELIA FROM JAPAN TO THE WORLD. youtu.be/coG0ygtCghA". www.motivemediatz.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-05-23. Iliwekwa mnamo 2018-05-27.
  2. "Lister Elia.com | Welcome to Lister Elia's Official Web Site". www.listerelia.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-05-23. Iliwekwa mnamo 2018-05-27.
  3. Eddie Nassor (2015-01-12), Mziki wa dansi zilipendwa - MK Group - Maumivu makali, iliwekwa mnamo 2018-05-16
  4. TG producer (2015-05-13), KADIRI MKE WANGU by KYANGA SONGA,(Orch Sambulumaa),on Keyboards, Lister Elia., iliwekwa mnamo 2018-05-16
  5. TG producer (2016-05-17), MAYOMBO -Songwriter,Kasaloo Kyanga.On Keyboards,Lister Elia. Orchestra Sambulumaa., iliwekwa mnamo 2018-05-16
  6. TG producer (2017-04-02), The MK Group featuring Lister Elia's "MAPENZI YA ADHABU". Lister Elia on Keyboards., iliwekwa mnamo 2018-05-22
  7. TG producer (2015-05-12), Mama Happy " by Lister Elia (Orch Sambulumaa), iliwekwa mnamo 2018-05-20
  8. "MAHOJIANO KATI YA KAVASHA GROUP NA M-TANZANIA, JAZZ PIANIST/AUTHOR, LISTER ELIA". MAHOJIANO KATI YA KAVASHA GROUP NA M-TANZANIA, JAZZ PIANIST/AUTHOR, LISTER ELIA. ~ KAVASHA GROUP TANZANIA. 2016-02-23. Iliwekwa mnamo 2018-05-16.
  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lister Elia kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.