Christopher Charles Lloyd (Amezaliwa tar. 30 Aprili 1982), anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Lloyd Banks, ni rapa wa kimarekani na mmoja wa kundi la G-Unit.

Lloyd Banks
Jina Kamili {{{jina kamili}}}
Jina la kisanii Lloyd Banks
Nchi Marekani
Alizaliwa 30 Aprili 1982,
Aina ya muziki Rap na Hip hop
Kazi yake Mwanamuziki
Miaka ya kazi 1999 - hadi leo
Ameshirikiana na G-Unit, Eminem
Ala Sauti
Kampuni G-Unit, Interscope

Wasifu hariri

Maisha ya awali hariri

Lloyd Banks alizaliwa na mzee Christopher Lloyd mjini Baltimore, Maryland na akakulia mjini South Jamaica, Queens. Mama yake ni Mpuerto Rico na baba yake ni Mmarekani mweusi.

Wakati wazazi wa Banks wangali vijana hawakuwahi kuoana hadi alivyokuja kuzaliwa Banks. Baba yake aliambulia zaidi utoto wa Banks akiwa jela, na kumuacha Banks akilelewa na mama yake huku akiwa anapata msaada kutoka kwa ndugu wa baba wa Banks. Mamam yake Lloyd Banks alikuwa na kawaida ya kumuacha Lloyd akiwa anaangaliwa na kaka yake Lloyd pindi tu mama aendapo mizungukoni

Akiwa mdogo Banks alianza kuandika vitu vinanvyofanana na maishairi na kuanza kuvifanyia mazoezi. Kwa bahati nzuri Lloyd akapata moyo zaidi na kuanza kurap katika baadhi ya mitaa iliyopo mjini New York.

Kwakweli iliwagusa baadhi ya watu na kuanza kumshangaa Lloyd anavyo fanya mambo ya ajabu mtaanii hapo. Akawa anahifadhi baadhi ya mashari kisha anaenda kushiriki katika mashindano ya mtaani, huku akiwa anabuni nanma ya kuwavuta watu, pia na majigambo yasiyozulika na kuanza kujivumisha kuwa yeye ni mmbora zaidi.

Kuja kuwa maarufu hariri

Tony Yayo, ni mkubwa kiumri na anauzoefu katika muziki wa rap, alijiunga na 50 Cent katika safari ya kumtafutia soko Nas, Cash Money na Ruff Ryders. Banks yeye alibaki nyumbani akimsubiri 50 Cent na Yayo kurudi huko safarini. Banks yeye alianza kuimba mtaani huku akizunguka katika nyumba za majirani huku akizidi kujitamba mtaani.

Baadae alichukuliwa na mtaarishaji mmoja wa muziki wa jirani kwao na kuanza kutengeneza tepu za nyimbo mchanganyiko za kienyeji. Lloyd Banks ameanza kujulikana na kupewa heshima baada ya kutoa sini ya tepu mchanganyiko.

Albamu alizotoa hariri

Makala kuu ya albamu za Lloyd Banks

  • 2004: The Hunger for More
  • 2006: Rotten Apple
  • 2008: Gang Green

Marejeo hariri

  1. http://www.sixshot.com/3684/ Archived 3 Juni 2008 at the Wayback Machine.
  2. http://www.sing365.com/music/lyric.nsf/Lloyd-Banks-Biography/BFE96E13A180848B48256EC5000CF234 Archived 26 Oktoba 2007 at the Wayback Machine.
  3. http://www.g-unitsoldier.com/main.html
  4. http://www.askmen.com/men/entertainment_150/165c_lloyd_banks.html Archived 27 Februari 2008 at the Wayback Machine.

Viungo vya Nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:


  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lloyd Banks kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.