50 Cent
Curtis James Jackson III (amezaliwa tar. 6 Juni 1975) ni mwanamuziki wa rap-hip hop, mwigizaji na mtayarishaji kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama 50 Cent.
50 Cent | |
---|---|
50 Cent, mnamo 2006
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Curtis James Jackson III |
Amezaliwa | 6 Juni 1975 |
Asili yake | Queens, New York |
Aina ya muziki | Hip hop |
Kazi yake | Rapa Mwigizaji Mtayarishaji |
Studio | Jam Master Jay Records Columbia Records Aftermath Records G-Unit Records Interscope Records Shady Records Violator Records |
Ame/Wameshirikiana na | G-Unit Eminem Dr. Dre Mobb Deep Sha Money XL |
Tovuti | 50cent.com |
Ameanza kupata umaarufu zaidi baada ya kutoa albamu yake ya "Get Rich or Die Tryin" na 'The Massacre'. 50 Cent amepata Plantinam nyingi na mafanikio makubwa katika albamu zake mbili, aliuza nakala zaidi ya Mil. 21 kwa hesabu ya dunia nzima.
Masha ya awali na muziki
hariri50 Cent alizaliwa mjini South Jamaica, Queens ndani ya New York, Marekani. 50 Cent ameanza kujishughulisha na masuala ya uuzaji wa dawa za kulevya toka akiwa na umri wa miaka 12, hiyo ilikuwa kwenye miaka ya '80', akiwa anajushughulisha na masuala ya uuzaji wa dawa za kulevya. 50 Cent pia akawa anajaribu kidogo masuala ya muziki wa rap na hip hop.
50 Cent alipigwa risasi tisa mnamo mwaka 2000. Kadri miaka inavyozidi kwenda 50 Cent akabahatika kutoa tepu ya nyimbo mchanganyiko ilyokuwa inaitwa "Guess Who's Back?" mnamo mwaka wa 2002.
50 Cent aligunduliwa kipaji chake na mwanamuziki 'Eminem' na kumwingiza katika studio ya Interscope Records kwa msaada wa Eminem na Dr. Dre, ambaye ndiye aliye tayarisha albamu ya kwanza ya 50 Cent na kumpa mafanikio makubwa katika ulimwengu wa muziki.
Studio binafsi
haririMnamo mwaka 2003 50 Cent alianzisha Studio yake iitwayo G-Unit Records, ambayo iliingiza Marapa maarufu kama vile Young Buck, Lloyd Banks, na Tony Yayo, kitu ambacho kilipelekea kupata uhasama na chuki nzito na baadhi ya wasanii nchini marekani, moja kati ya wasanii hao ni Ja Rule, The Game, na Fat Joe. Pia 50 Cent alikuwa akiibia masuala ya uigizaji na kuonekana kwenye baadhi ya filamu zenye kuhusu albamu yake na filamu illitwa "Get Rich or Die Tryin" na akashiriki pia kwenye filamu ya "Iraq War" na filamu ya "Home of the Brave" iliyotoka mwaka 2006.
Albamu alizotoa
hariri- 2003: Get Rich or Die Tryin'
- 2005: The Massacre
- 2007: Curtis
- 2009: Before I Self Destruct
Filamu alizotoa
haririMwaka | Jina la Filamu | Jina Aliotumia | Maelezo |
---|---|---|---|
2003 | 50 Cent: The New Breed | 50 Cent | Makala za Documentary DVD |
2005 | "Pranksta Rap" | 50 Cent | The Simpsons Sehemu ya 16.9 |
Get Rich or Die Tryin' | Marcus | Toleo la Motion picture | |
50 Cent: Bulletproof | 50 Cent | Video game, Sauti tu. | |
2006 | Home of the Brave | Jamal Aiken | |
2007 | The Dance | — | |
2008 | The Ski Mask Way | Seven | Ipo kwenye Maandalizi |
Righteous Kill | — | Inatengenezwa | |
Live Bet | — |
Tuzo alizopata
haririViungo vya nje
hariri- Tovuti Binafsi ya 50 Cent
- 50 Cent Archived 17 Desemba 2008 at the Wayback Machine. Katika AOL Sessions
- 50 Cent Archived 11 Machi 2008 at the Wayback Machine. Katika MTV