George Byron

(Elekezwa kutoka Lord Byron)

George Gordon Byron, 6th Baron Byron (22 Januari 178819 Aprili 1824) alikuwa mshairi na mwandishi mashuhuri nchini Uingereza. Mara nyingi anatajwa kwa cheo chake cha kikabaila kama Lord Byron.

Byron

Alikuwa mrithi wa mali kubwa hivyo aliweza kuendesha maisha kufuatana na mapenzi yake tu. Alikuwa maarufu kwa wapenzi wake wengi. Pamoja na kuandika alisafiri mahali pengi katika nchi za Bahari ya Mediteranea.

Tangu 1816 alihamia Italia alipojiingiza katika kundo la kisiasa lililolenga kuanzisha mapinduzi dhidi ya utawala wa Austria katika Italia ya Kaskazini. Aliamriwa kukaa katika mji wa Pisa bila kibali cha kutoka nje akatumia muda kwa mashairi.

1823 alipokea wito kutoka Ugiriki akawa kiongozi wa jeshi la Wagiriki waliopigania vita ya Uhuru dhidi ya Waturuki Waosmani. Hapa alikufa 1824 baada ya kungonjeka. Wagiriki wanamkumbuka hadi leo kama msaidizi wa uhuru wao.

Kazi zake

hariri

Kazi ndogo

hariri

Viungo vya Nje

hariri
 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
 
WikiMedia Commons



  Makala hii kuhusu mwandishi fulani wa Ulaya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu George Byron kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.