Louise Guthrie

Msanii wa Afrika ya Kusini

Louise Guthrie'alizaliwa mnamo tareh ' (10 Oktobamwaka 1879 - had 20 Februari 1966) alikuwani ni mtaalamu wa mimea na msanii wa mimea wa Afrika Kusini.

Louise Guthrie
Jina la kuzaliwa Louise
Alizaliwa 10 Oktoba 1879
Alikufa 20 Februari 1966
Nchi Afrika Kusini
Kazi yake Msanii na Mtaalamu wa Mimea

Maisha ya Awali na Elimu

hariri

Isobel Louise Sophie Guthrie alizaliwa mnamo mwaka 1879 Cape Town nchini Afrika Kusini, binti wa Profesa wa mimea na hisabati aliyezaliwa Uingereza Francis Guthrie pamoja na mkewe Isabella Grisbrook.[1] Alisoma katika shule ya Rustenburg Girls High School.[2]

Louise Guthrie alikuwa msaidizi wa mimea huko Bolus Herbarium, kuanzia mwaka 1918, hadi mwaka 1927. Alipokuwa huko, aliendeleza ustadi wake kama mchoraji mimea, anayejulikana zaidi kwa safu ya maonyesho 264 ya spishi protea iliyopatikana nchini Afrika Kusini, iliyoanza mnamo mwaka 1925, na ya mwisho ya mwaka 1947. Alitoa zawadi kwa Bolus Herbarium katika mwaka 1948[2]

Maisha ya binafsi na urithi

hariri

Jina la mmea wa guthriae linampa heshima kubwa Louise Guthrie.[3] Sanaa yake imehifadhiwa kwenye Chuo Kikuu cha Cape Town. Jumuiya ya mimea ya Hermanus ilifanya maonyesho ya uchoraji 76 na Guthrie mnamo mwaka 2000 huko Fernkloof hifadhi ya asili. Baadhi ya rangi zake za maji zinaonyeshwa kwenye Nyumba ya Afrika Kusini huko London.[2]

Marejeo

hariri
  1. Mary Gunn and L. E. W. Codd, eds., Botanical Exploration of Southern Africa (CRC Press 1981): 175-176. ISBN|9780869611296
  2. 2.0 2.1 2.2 John P. Rourke. "A Passion for Proteas: The Botanical Art of Louise Guthrie" Archived 3 Februari 2016 at the Wayback Machine. Veld & Flora 87(September 2001): 120-123.
  3. Urs Eggli and Leonard E. Newton, eds., Etymological Dictionary of Succulent Plant Names (Springer Science & Business Media 2013): 100. ISBN|9783662071250
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Louise Guthrie kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.