Lucas Cranach Mzee
Lucas Cranach Mzee (tamka: "Lukas Kranakh"; 1472–16 Oktoba 1553) alikuwa mchoraji na mkata nakhshi Mjerumani. Anaitwa "Mzee" kwa kusudi la kumtofautisha na mwanawe msanii mwenye jina lilelile anayejulikana kama "Lucas Cranach Kijana".
Maisha
haririAlizaliwa katika mji mdogo wa Kronach katika eneo la Frankonia, Bavaria. Babake Hans alikuwa mchoraji pia lakini hakuna habari zaidi juu yake. Lucas alijiita kufuatana na mji Kronach alikozaliwa kwa umbo la kilatini "Cranach". Baada ya kujifunza uchoraji -labda kwa babake- alienda kwenye safari ya ufundistadi iliyokuwa kawaida kwa fundi kijana siku zile kuzunguka nchini na kujifunza mbinu mpya mahali mbalimbali.Kazi zake za kwanza zinajulikana kutoka kipindi alipokaa mjini Vienna.
Mwaka 1505 alipewa ajira kama mchoraji rasmi kwenye ikulu ya mtawala Frederik III wa Saksonia mjini Wittenberg. Kazi yake ilikuwa hasa kuchora taswira kwa ajili ya makanisa na maboma ya Saksonia. Pamoja na hayo alianza kuchapisha pia michoro kwa njia ya utiaji nakshi au mihuri ya mbao na kuiuza.
Mwaka 1508 mtawala wake alimpa haki ya kutumia nembo ya binafsi iliyokuwa nyoka mwenye mabawa anayeshika pete mdomoni.Kutokana na ubora wa kazi yake mtawala Frederik III alimtuma Lucas kwenda kwenda Uholanzi alipochora taswira za Kaisari Maxilimilian I na mwanawe aiyemfuata baadaye kama Kaisari Karolo V.
Mnammo 1512 alimwoa Barbara Brengebier († 25. Dezember 1540) akaza naye wavulana 2 na mabinti 3. Pamoja na kazi yake ya kisanii alitumia mapato yake kuanzisha pia miradi mbalimbali kama hoteli na maduka la madawa, vitabu, karatasi na mengine. Mara kadhaa alichaguliwa kama mtunza hazina na baadaye pia kama meya wa manisipaa ya Wittenberg. Hapo Wittenberg alikuwa karibu na vyanzo vya matengenezo ya kiprotestanti akawa rafiki wa Martin Luther na Philipp Melanchthon. Pamoja na mkewe alikuwa shahidi kwenye arusi ya Martin Luther na Katharina wa Bora.
Kazi
haririLucas Cranach Mzee aliendelea kuwa kati ya wachoraji mashuhuri wa Ujerumani na Ulaya wa karne yake. Sehemu kubwa ya taswira zake ni picha za watu hasa watawala lakini pia watu raia. Kutokana na picha zake tunajua uso wa Martin Luther na watu wengine wa wakati wake. Alichora pia picha za Biblia na baada ya kufahamiana na Luther taswira mbalimbali zilizotangaza ujumbe wa kipotestanti. Hata hivyo aliendelea kupokea wateja wakatoliki wlaiotaka picha yao kutoka mkono wake. Aina nyingine za picha ni michoro na taswira zinasimulia hadithi za Waroma wa Kale jinsi ilivyokuwa kawaida wakati ule wa renaissance. Hapa alichora mara kwa mara mabinti uchi kufuatana na mifao wa wasanii wa Italia.
Cranach alisimamia karahana kubwa penye wachoraji wengine. Mara nyingi alianzisha picha akikazia muundo wa taswira na kuwaachia watu wengine kujaza rangi na sehemu za kando za picha.
Kifo
haririLucas Cranach Mzee aliaga dunia 16 Oktoba 1553 mjini Weimar, Ujerumani. Nyumba yake iko hadi leo kwenye uwanja wa soko wa mji.
Baadhi za kazi zake
hariri-
Mapumziko njiani ya kukimbilia Misri (1504)
-
Binti mkabaila wa Saksonia, mnamo 1517
-
Johannes Cuspinian, 1503
-
Philipp Melanchthon
-
Pepo wa maji, akipumzika , 1530
-
Johann Friedrich mtawala wa Saksonia, 1531
-
Judiht akishika kichwa cha Holofernes
-
Mariamu na Yohane chini ya msalaba
-
"Mpinzani wa Kristo", 1521
References
hariri- Posse, Hans (1942) Lucas Cranach d. ä. A. Schroll & Co., Vienna OCLC 773554 in German
- Descargues, Pierre (1960) Lucas Cranach the Elder (translated from the French by Helen Ramsbotham) Oldbourne Press, London, OCLC 434642
- Ruhmer, Eberhard (1963) Cranach (translated from the German by Joan Spencer) Phaidon, London, OCLC 1107030
- Friedländer, Max J.and Rosenberg, Jakob (1978) The Paintings of Lucas Cranach Tabard Press, New York ISBN 0-914427-31-8
- Schade, Werner (1980) Cranach, a Family of Master Painters (translated from the German by Helen Sebba) Putnam, New York, ISBN 0-399-11831-4
- Stepanov, Alexander (1997) Lucas Cranach the Elder, 1472-1553 Parkstone, Bournemouth, England, ISBN 1-85995-266-6
- Koerner, Joseph Leo (2004) The reformation of the image University of Chicago Press, Chicago, ISBN 0-226-45006-6
- Moser, Peter (2005) Lucas Cranach: His Life, His World, His Pictures (translated from the German by Kenneth Wynne) Babenberg Verlag, Bamberg, Germany, ISBN 3-933469-15-5
- Brinkmann, Bodo et al. (2007) Lucas Cranach Royal Academy of Arts, London, ISBN 1-905711-13-1