Kaizari Karoli V
(Elekezwa kutoka Kaisari Karolo V)
Karoli V (pia: Carlos I wa Hispania[1]; 24 Februari 1500 – 21 Septemba 1558) alikuwa Kaizari wa Dola Takatifu la Kiroma[2] kuanzia 1519 hadi kujiuzulu mwezi wa Septemba 1556.
Alimfuata babu yake, Maximilian I, na kufuatiwa na mdogo wake Ferdinand I.
Kwa jina la Carlos I alikuwa mfalme wa kwanza wa Hispania tangu mwaka 1516. Kwa kuwa nchi hiyo ilikuwa na makoloni mengi hasa barani Amerika, aliweza kusema, "Katika ufalme wangu jua halitui kamwe".
Marejeo
hariri- ↑ Karoli, Carlos, Karl, Charles, Carlo, ni maumbo tofauti ya jina lilelile la asili ya Kigermanik katika lugha mbalimbali za Ulaya
- ↑ Dola Takatifu la Kiroma lilikuwa jina la milki iliyounganisha Ujerumani, Uholanzi, Ubelgiji pamoja na maeneo kadhaa ya Italia, Ufaransa na Ucheki wa leo katika enzi ya kati hadi 1806.
Makala hii kuhusu Kaizari fulani wa Ujerumani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kaizari Karoli V kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |