Vienna (Kijer.: Wien) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Austria. Iko katika mashariki ya Austria kando la mto Danubi. Idadi ya wakazi imezidi milioni moja na lakhi sita. Vienna ina cheo cha jimbo ndani ya shirikisho la jamhuri ya Austria.

Sehemu za Mji wa Vienna
Vienna

Bendera

Nembo
Vienna is located in Austria
<div style="position: absolute; z-index: 2; top: Expression error: Unexpected < operator.%; left: Expression error: Unexpected < operator.%; height: 0; width: 0; margin: 0; padding: 0;">
Vienna
Vienna
Mahali pa mji wa Vienna katika Austria
Majiranukta: 48°12′N 16°22′E / 48.2°N 16.367°E / 48.2; 16.367
Nchi Austria
Jimbo Vienna
Idadi ya wakazi
 - 1,680,000
Tovuti: www.wien.gv.at
Vienna

UtawalaEdit

Vienna imegawiwa katika mitaa 23.

 1. Innere Stadt (Kitovu cha jiji)
 2. Leopoldstadt
 3. Landstraße
 4. Wieden
 5. Margareten
 6. Mariahilf
 7. Neubau
 8. Josefstadt
 9. Alsergrund
 10. Favoriten
 11. Simmering
 12. Meidling
 13. Hietzing
 14. Penzing
 15. Rudolfsheim-Fünfhaus
 16. Ottakring
 17. Hernals
 18. Währing
 19. Döbling
 20. Brigittenau
 21. Floridsdorf
 22. Donaustadt
 23. Liesing

UtamaduniEdit

 
Kanisa Kuu la Mt. Stefano ni kati ya majengo mashuhuri ya Vienna.

Kwa karne nyingi Vienna ilikuwa mji mkuu wa dola kubwa. Wafalme na makaisari wa familia ya Habsburg walitawala Dola Takatifu ya Kiroma hadi 1806 na baadaye na maeneo makubwa ya Ulaya ya kusini-mashariki hadi 1918. Hivyo Vienna ina majengo mazuri inayotunza kumbukumbu ya enzi za kale sio tu mji mkuu wa Austria ndogo ya leo.

Watu wa Vienna hukumbuka wasanii walioishi katika mji wao kama watunga muziki Wolfgang Amadeus Mozart, Ludwig van Beethoven na Brahms.

Viungo vya NjeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Austria bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Vienna kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. 
Majimbo ya Austria
 
Austria Chini (Niederösterreich)Austria Juu (Oberösterreich)BurgenlandKarinthia (Kärnten)SalzburgSteiermarkTirolVienna (Wien)Vorarlberg