Lugha ya maandishi

Tofauti kati ya lugha ya maandishi na lugha ya mazungumzo ni kama:

1.Ubora wa lugha ya maandishi hutegemea vifaa vya kutaipu au hati ya mwandishi ila ubora wa mazungumzo hutegemea ubora wa sauti ya mzungumzaji

2.Lugha ya maandishi haina hadhira ila lugha ya mazungumzo ina hadhira.

Sifa za lugha ya maandishi hariri

  • lugha ya maandishi huweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu.
  • lugha ya maandishi hutumia njia maalumu, kwa mfano gazeti.
  • lugha ya maandishi ni lugha isiyoonesha uhalisia wa hisia za mzungumzaji
  • lugha ya maandishi ni lugha inayotolewa kwa gharama.

Tofauti kati ya lugha ya maandishi na lugha ya mazungumzo hariri

  • lugha ya maandishi inatumia gharama lakini lugha ya mazungumzo haitumii gharama.
  • lugha ya maandishi huweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu lakini lugha ya mazungumzo haiwezi kuhifadhiwa kwa muda mrefu.
  • lugha ya maandishi haioneshi uhalisia wa hisia za mzungumzaji lakini lugha ya mazungumzo inaonesha hisia za mzungumzaji.
  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lugha ya maandishi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.