Kislavoni cha Kusini
(Elekezwa kutoka Lugha za Kislavoni za Kusini)
Kislavoni cha Kusini ni kundi la lugha za Kislavoni zinazozungumzwa kwenye Balkani (Ulaya ya Kusini-Mashariki).
Idadi ya wasemaji wa lugha hizi ni ni takriban milioni 34. Mwandiko hutumia alfabeti ya Kisirili upande wa mashariki (Kibulgaria, Kiserbia, Kimasedonia) na alfabeti ya Kilatini upande wa magharibi (kama vile Kikroatia, Kislovenia). Kiserbokroatia kiliandkiwa kwa namna zote mbili.
Lugha hizi zimetengwa na eneo la wasemaji wengine wa Kislavoni kwa kanda lenye wasemaji wa Kijerumani (Austria), Kihungaria na Kiromania.