Lulu (Siri ya Mtungi)
Lulu ni jina la uhusika kutoka katika tamthilia ya Siri ya Mtungi kutoka nchini Tanzania. Uhusika umechezwa na Yvonne Cherry. Toto la mjini, halishindwi kitu. Fundi wa mipango halali na isiyo halali. Mwenye kujiingiza kwenye kila sekta. Sifa pekee aliyonayo shangingi Lulu ni kuwa, hakuna mwanaume anayeweza kumkataa. Tena kwa gharama yoyote ile. Amecheza kama mpango wa kando wa Cheche Mtungi. Uhusika wake hasa unahusu mwanamke machepele mwenye uwezo wa kifedha. Amenunua kila aliyejaribu kufuatilia nyendo zake. Kazi yake hasa haijulikani, licha ya kuonekana anaishi katika jumba la kifahari lililopo ufukweni mwa bahari.
Lulu | |
---|---|
muhusika wa Siri ya Mtungi | |
Taswira ya Lulu (Siri ya Mtungi) (uhusika umechezwa na Yvonne Cherry) | |
Imebuniwa na | MFDI Tanzania |
Imechezwa na | Yvonne Cherry |
Misimu | 1, 2 |
Maelezo | |
Jinsia | Kike |
Kazi yake | Tapeli wa mjini Mlaghai wa mapenzi |
Utaifa | Mtanzania |
Kulingana na tabia yake, dhahiri ni mchepuko wa vigogo. Mwenye kujihusisha ma mipango mingi tu mjini pale, Bagamoyo. Lulu ni mwanamke gumzo sana na mwenye kuogopwa na wanawake wa mji wake, hasa kwa kuwa na hofu ya kuchukuliwa wuame zao. Pamoja na uzuri na ushawishi alionao, Cheche kwa msaada wa kimawazo kutoka kwa Dafu, alifanikiwa kumkataa Lulu mchana kweupe.
Kwa figisu tu, hajambo. Alitengeneza mazingira ya kuwa meneja wa Mtungi Studio baada ya Shalimar kurudi kutoka Kanada. Figisu hii ilizua taharuki kubwa katika ndoa ya Cheche. Dhumuni hasa la kumleta Lulu katika studio ilikuwa kuhakikisha Cheche anapiga picha anazozitaka Shalimar kwa ajili ya wakala wa ulimwende na mitindo kutoka sehemu mbalimbali.
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ Lulu (Siri ya Mtungi) Ilihifadhiwa 12 Septemba 2016 kwenye Wayback Machine. katika wavuti rasmi ya Siri ya Mtungi.