Lyon ndiyo mji mkuu wa mkoa wa Rhône-Alpes na wa tatu katika Ufaransa nzima. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2007, mji huu pamoja na vitongoji vyake una wakazi wapatao milioni 4.4. Mji upo mita 162-312 juu ya usawa wa bahari.

Mji wa Lyon
Jiji la Lyon
Jiji la Lyon is located in Ufaransa
Jiji la Lyon
Jiji la Lyon
Mahali pa mji wa Lyon katika Ufaransa
Majiranukta: 45°45′1″N 4°50′3″E / 45.75028°N 4.83417°E / 45.75028; 4.83417
Nchi Ufaransa
Mkoa Rhône-Alpes
Wilaya Rhône
Idadi ya wakazi (2006)
 - 1,783,400
Tovuti: www.lyon.fr
Fourvière

Lyon katika historiaEdit

Kihistoria ni muhimu tangu zamani, kwa kuwa ulikuwa mji mkuu wa Gallia. Kiini cha mji kimeorodheshwa na UNESCO mwaka 1998 katika Urithi wa dunia.

Kutoka huko Ukristo ulienea katika nchi inayoitwa sasa Ufaransa. Ndiyo sababu askofu wake anahesabiwa mpaka leo kuwa mkuu kuliko wale wote wa nchi hiyo. Maarufu kati ya watakatifu wake: wafiadini wa Lyon na askofu Ireneo.

Katika karne ya 13 mjini ilifanyika mitaguso miwili inayohesabiwa na Kanisa Katoliki kuwa mitaguso mikuu: Mtaguso I wa Lyon (1245) na Mtaguso II wa Lyon (1274). Mpaka leo jimbo hilo linadumisha mambo machache ya pekee katika liturujia kufuatana na mapokeo ya Gallia (Liturujia ya Lyon).

Tazama piaEdit

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ufaransa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Lyon kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.