Baharia : Tofauti kati ya masahihisho

Mtu anaefanya kazi kwenye meli,mashua au jahazi
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|Mabaharia wakiangalia kung'oa kwa nanga wakati wa kutoka bandarini Picha:Deck...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 10:24, 25 Mei 2017

Baharia, pia mwanamaji ni mtu anayefanya kazi kwenye chombo cha usafiri majini, hasa baharini kama vile boti, mashua, jahazi au meli.

Mabaharia wakiangalia kung'oa kwa nanga wakati wa kutoka bandarini
Mabaharia Wajerumani kwenye kazi ya usafi wa sitaha kwenye jahazi mnamo 1958

Kuna kazi nyingi tofauti zinazotekelezwa na mabaharia. Mkuu wao ni nahodha au kapteni wa chombo. Katika mashua au jahazi ndogo mabaharia wote wanafanya kazi pamoja ilhali kazi sahili na ngumu zaidi hupewa kwa wale walio vijana. Kadri jinsi meli ni kubwa zaidi shughuli zinagawiwa baina ya mabaharia wenye ufundi fulani.

Meli kubwa unaweza kuwa na idara tofauti kama vile

  • shughuli za sitaha pamoja na mizigo
  • shughuli za injini
  • huduma za chakula
  • huduma ya afya

Hapo kapteni atakuwa na kundi la maafisa wake wanaosimamia idara mbalimbali baada ya kupita kwenye mafunzo na mitihani maalumu kwa ajili ya shughuli zao.

Viungo vya Nje