Mlangobahari wa Taiwan : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|Ramani ya Mlangobahari wa Taiwan thumb|Taiwan Strait '''Mlangobahari...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 19:24, 7 Oktoba 2019

Mlangobahari wa Taiwan (ing. Taiwan Strait au Formosa Strait) ni sehemu ya bahari iliyopo kati ya China bara na kisiwa cha Taiwan. Huu ni mlangobahari unaounganisha Bahari ya Mashariki ya China na Bahari ya Kusini ya China. Upana wake ni kilomita 180, sehemu nyembamba kabisa km 131.

Ramani ya Mlangobahari wa Taiwan
Taiwan Strait

Ni njia ya bahari inayotumiwa na meli nyingi sana zinazobeba kontena baina ya mabandari ya China bara.

Tangu ushindi wa ukomunisti katika China bara kwenye mwaka 1949 mlangobahari huu uliona mapambano kadhaa ya kijeshi. Jeshi la Kuomintang chini ya rais Chiang Kai-shek liliweza kujiokoa mbele ya Wakomunisti chini ya Mao Zedong wakivuka bahari wakafaulu kujitetea pale Taiwan na pia kwenye visiwa vidogo karibu na pwani la bara. Jeshi la ukombozi la watu wa China lilipiga mizinga visiwa vya karibu kama Qemoy kwa miaka mingi. Kwa jumla manowari za Marekani zilizuia mashambulio ya jeshi la bara kufika Taiwan. 1965 kulikuwa na mapigano kahdaa baina ya manowari wa pande zote mbili katika eneo la mlangobahari.

Baada ya Jamhuri ya Watu wa China kupokelewa 1972 katika Umoja wa Mataifa mashambulio katika mlangobahari yalikwisha. Baada ya kifo cha Mao na siasa mpya chini ya Deng Xiaoping biashara iliweza kuanza baina pande hizi mbili za China, mwanzoni kwa umbo la magendo na baadaye pia kwa njia halali. Leo hii watalii na wafanyabiashara kutoka pande zote mbili za mlangobahari wanavuka na kutembelea upande mwingine.

Wikimedia Commons ina media kuhusu: