Chiang Kai-shek alikuwa mwanajeshi na mwanasiasa nchini China. Aliongoza nchi kati ya 1927 na 1949 aliposhindwa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe ya China.

Jenerali na Rais Chiang Kai-shek 1945
Chiang Kai-shek kama rais wa China

Alizaliwa 31 Oktoba 1887 karibu na Shanghai akajiunga na chama cha Kuomintang. Baada ya kifo cha Sun Yat-sen alichukua uongozi wa Kuomintang na kuungunisha China kijeshi. Tangu 1949 alikaa kisiwani Taiwan alipoongoza serikali ya Jamhuri ya China. Aliaga dunia 5 Aprili 1975 mjini Taipei.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chiang Kai-shek kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.