Maarifa (kutoka Kiarabu; kwa Kiingereza: competence) ni njia inayotumiwa kujitoa katika shida ama kuweza kupata kitu, kwa kutumia elimu au ujuzi; pia huhusisha Ufahamu na uelewa, hususani wa ukweli kama ulivyofundishwa au kuthibitishwa na Roho.

Ujuzi huo unaweza ukawa wa kuzaliwa nao au ukatokana na mang'amuzi ya maisha yakiwa pamoja na kusoma, kusikia au kutenda.

Neno hilo linatumika pia kudokeza mbinu za ushirikina katika kufanikisha mambo kadiri ya matakwa ya mtu.