Madeline Kimei

Mtaalamu wa sheria wa Tanzania, msuluhishi na mpatanishi anayetekeleza sheria za biashara na ushirika.


Madeline Kimei ni mwanamke mwanasheria kutoka nchini Tanzania na mwanamke wa kwanza kuanzisha jukwaa la kidijitali la kisheria ili kusuluhisha migogoro ya kisheria, jukwaa hilo linaitwa iResolve. Ni mwanasheria wa kujitegemea aliye na uzoefu katika kutoa misaada ya kisheria hasa katika usuluhishaji wa migogoro.[1][2]

Madeline Kimei
Amezaliwa
Tanzania
Nchi Tanzania
Kazi yake Mwanasheria

Maisha ya awali

hariri

Madeline alisoma katika chuo kikuu cha Conventry cha nchini Uingereza na kupata shahada yake ya kwanza katika sheria LLB, pia alipata shahada yake ya uzamivu katika chuo kikuu cha Bournemouth cha nchini uingereza. Madeline alipata stashahada katika mambo ya sheria katika taasisi ya Arbitration ya nchini uingereza. Ana cheti cha usuluhishi kutoka katika taasisi ya moja ya nchini India ya Arbitration and Mediation. Amekuwa mwanachama wa chama cha wasuluhishaji cha nchini Tanzania tangu mwaka 2011 na kutumikia chama hicho kama mwenyekiti msaidizi wa chama hicho tangu mwezi Juni 2016. Ni mwanamke mbobezi na mwenye uzoefu katika sheria ya usuluhishaji ya UNCITRAL Rules for Arbitration the ICC Rules and TiArb Arbitration Rules.[3]

Madeline aliwahi hufanya kazi na benki ya stanbic na NBC katika nyazifa mbalimbali za kisheria.

Tuzo/Mafanikio yake katika Nyanja ya Sheria

hariri

Madeline amewahi kutajwa kama mwanamke mwenye uzoefu na mambo ya kisheria kama mshauri wa mikataba ya kisheria, uwezeshaji na uendeshaji wa makubaliano ya mikataba ya kisheria, na FIDIC. Pia kama mshauri wa maswala ya miamala ya fedha, kisheria.[4]

Mwaka 2015 alitunukiwa kama mwanachama bora wa kituo cha utafiti wa kisheria kwa ushirikiano wa China na Afrika kijulikanacho kama China-Africa Research Centre and Consultant, pia katika taasisi nyingine kama Centre for Legal Diplomacy, Legal Training Base na The FOCAC China Africa Legal Cooperation Forum. [5] Madeline amejikita sana katika kupanua uelewa wa watu hasa Watanzania katika maswala ya usuluhishaji wa migogoro.Amefanya kazi kama Katibu mkuu wa bodi ya benki ya Stanbic Bank Tanzania tangu mwaka 2010 mpaka 2012.

Kama mshauri wa maswala ya kisheria katika bodi ya benki ya National Bank of commerce Ltd (NBC) tangu mwaka 2013 mpaka 2015.[6]

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Madeline Kimei kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Marejeo

hariri
  1. http://www.sheroes.co.tz/sheroes.html Ilihifadhiwa 8 Machi 2019 kwenye Wayback Machine. iliangaliwa tar 7 March 2019
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-03-08. Iliwekwa mnamo 2019-03-07.
  3. https://allafrica.com/stories/201507140756.html
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-03-07. Iliwekwa mnamo 2019-03-07.
  5. https://www.ippmedia.com/en/business/lawyers-given-basics-ofinternational-commercial-arbitration
  6. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-03-08. Iliwekwa mnamo 2019-03-07.