Mahimbi
Mahindi ni aina ya chakula chenye kufanana na magimbi.
Zao hili hulimwa katika maeneo yenye maji, hasa karibu na mito au majaruba, kwani zao hili hupendelea sana maji pamoja na hali ya hewa ya ubaridi.
Chakula hiki hupendelewa kuliwa zaidi na Waluguru hasa waishio milimani yaani maeneo ya kuanzia Mgeta, Nyandira pamoja na Tchenzema.
Chakula hiki, ambacho huliwa zaidi kipindi cha kuanzia mwezi wa tatu na kuendelea, hutakiwa kupikwa kwa umakini mkubwa sana, kwani kisipoiva vizuri kinaweza kuleta madhara kwa mlaji, kama kuwashwa kooni na mdomoni au kuvimba mdomo.
Katika Tanzania zao hili hulimwa pia katika maeneo ya Kilimanjaro, Manyara na Tanga.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |