Mkoa wa Manyara

Mkoa wa Manyara ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 27000. Umepakana na mikoa ya Arusha na Kilimanjaro upande wa kaskazini, Mkoa wa Tanga upande wa mashariki, Mkoa wa Dodoma upande wa kusini na mikoa ya Singida na Shinyanga upande wa magharibi.

Mkoa wa Manyara katika Tanzania
Wilaya za Mkoa wa Manyara

Mkoa wa Manyara umetengwa na Mkoa wa Arusha mwaka 2002 kwa azimio la rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukiwa na eneo la km² 46,359.

Babati ndiyo makao makuu ya mkoa.

WakaziEdit

Jumla ya wakazi mkoani ilikuwa 1,892,502 katika sensa ya mwaka 2022[1].

Idadi hiyo imepatikana katika wilaya zifuatazo (idadi ya wakazi katika mabano mwaka 2002): Babati (303,013), Hanang (205,133), Mbulu (237,882), Simanjiro (141,676) na Kiteto (152,757).

Sensa zinaonyesha kwamba ni kati ya mikoa ya Tanzania yenye ongezeko kubwa la wakazi. Pia ni kati ya mikoa yenye maambukizi machache zaidi ya Ukimwi.

Wenyeji wa mkoa huu ni pamoja na Wairaqw, Wamasai, Wambugwe, Wafyomi na Wabarbaig wakijihusisha na shughuli za kilimo na ufugaji kama njia ya kuingiza kipato chao cha kila siku.

WilayaEdit

Kuna wilaya zifuatazo: Babati, Mbulu, Hanang, Simanjiro and Kiteto.

Majimbo ya bungeEdit

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi 7 yafuatayo:

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

Viungo vya njeEdit