Mgeta ni tarafa ya uwanda wa juu (hadi mita 2,200 na zaidi juu ya UB) katika wilaya ya Mvomero, mkoa wa Morogoro, Tanzania yenye Postikodi namba 67321.

Ndiyo sehemu ambayo Waluguru wa mwanzo walitokea huko.

Ni sehemu inayosifika sana kwa kilimo cha mboga na matunda, kwa mfano njegere, maharage, mahindi, magimbi na viazi mviringo. Pia ndipo soko kubwa la matunda na mbogamboga lilipo Nyandila.