Majadiliano:Joel Joseph

Latest comment: miaka 6 iliyopita by Kipala

Makala hii imetungwa na mwenyewe ambayo haiwezekani hapa wikipedia. Azimio la kuipendekeza kwa ufutaji si rahisi. Sehemu za makala zingeweza kukubaliwa lakini nyingine ni kama tangazo. Ungekuwa huru kuweka maudhui yote na zaidi juu yako kwenye ukurasa wako wamajadiliano. Fuata majadiliano kwenye ukurasa wa Wikipedia:Makala_kwa_ufutaji#Joel_Joseph. Kipala (majadiliano) 15:20, 5 Julai 2018 (UTC)Reply

Sikh chache zilizopita katika Wikipedia ya kiingereza nilipata hii ukura ya Joel Joseph na ilikuwa na makosa mengi kweli. Ukurasa huu unakiuka maudhui ya Wikipedia na hufai kuwa hapa kamwe BrantleyIzMe (majadiliano) 18:30, 5 Julai 2018 (UTC)Reply

Kibaka Unadhani unaweza kutetea hoja? Kifupi hivi, kijana ni kweli ana ubora wa vyote alivyoandika. Je, ni dhani kwa mwanawikipedia mmoja maarufu aliyeamua kujiandika na kuitumikia Wikipedia? NAWAZA kwa maapana namana ya kujibu hoja hizi. Wapo wanawikipedia wanaochangia na kuwa na makala zao. Japo sheria zipo, na zikavunjwa huko mawikipedia makubwa. Tazama HAPA orodha ya wanawikipedia wenye makala. Ni kweli mwandishi, ni kweli mjasiriamali, ni kweli meneja wa Harmonize. Kuna shida? --Muddyb Mwanaharakati Longa 06:47, 6 Julai 2018 (UTC)Reply
Si kitu kama kuna wanawikipedia wenye makala zao. Labda siku moja pia makala yako? Ila tu hao ni watu wenye kiwango cha umaarufu ili wametambuliwa na wengine, walionekana katika vyanzo vya kukubalika na wengine waliamua kutunga makala. Kamwe hao wenyewe. Hatuna orodha ya watu waliojaribu kutunga makala zao, lakini kama ingekuwepo ingekuwa ndeeeefu sana. ila tu makala hizi zimefutwa zote (isipokuwa wajanja waliokuwa hodari kujificha). Kipala (majadiliano) 10:49, 6 Julai 2018 (UTC)Reply
Kipala Hapo sasa mtihani. Babu huishiwi maneno! Ngoja tuone utetezi wake!--Muddyb Mwanaharakati Longa 14:02, 6 Julai 2018 (UTC)Reply
Yuko huru kuweka jinsi anavyotaka kwenye ukurasa wake wa mtumiaji. Ilhali nimeshawaambia watu wengi maneno haya mara nyingi - je sasa iwe tofauti? Kipala (majadiliano) 14:12, 6 Julai 2018 (UTC)Reply
Rudi kwenye ukurasa wa " Joel Joseph ".