Wikipedia:Makala kwa ufutaji
Wikipedia:Makala kwa ufutaji (jamii MKU) ni mahali ambapo wanachama au wahariri wa Wikipedia hujadili kama makala inastahili kufutwa. Makala zilizoorodheshwa hupitia mjadala baadaye, zoezi la kufuta linaendelea kulingana na maoni ya jumuiya. Matokeo ya kawaida ya MKU ni pamoja na: makala kuendelea kuwepo, kuunganishwa na makala nyingine, kupelekwa tena kwa ukurasa mwingine (redirect), kuhifadhiwa kwa ajili ya marekebisho (incubation), kubadilishwa jina au kuwekwa kwenye kichwa kipya, kuhamishiwa kwenye ukurasa wa mtumiaji, au kufutwa kwa kufuata sera za kufuta. Pia, kurasa za kutoeleweka (disambiguation) pia hupendekezwa kufutwa katika MKU.
Majadiliano ya awali yamehamishwa kwenye kurasa hizi:
- Nyaraka 1 (2006-2010)
- Nyaraka 2 (2011-2013)
- Nyaraka 3 (2014)
- Nyaraka 4 (2017-18)
- Nyaraka 5 (2019)
- Nyaraka 6 (2020-21)
- Nyaraka 7 (2022 hadi 03/2023, zilizofutwa au kurekebishwa pekee)
- Nyaraka 8 (2021-25)
Utaratibu wa ufutaji
haririKama yeyote anaona makala haifai, ataweka msimbo wa }}futa{{ au kigezo kingine cha kufuta makala juu ya makala na kutaja sababu zake
- a) kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala na
- b) chini kwenye ukurasa huu kwa kuanzisha sehemu mpya chini ya kichwa ==[[JINA LA MAKALA INAYOTAJWA KWA UFUTAJI]]==.
- Azimio la kufuta si la huyu aliyeileta, ataamua mwingine. Tusubiri siku kadhaa ili mtunga makala au wengine wanaweza kuitetea au kuboresha. Tusifute haraka mno ili tusikatishe moyo wachangiaji wenzetu.
- Isipokuwa uharabu unaoeleweka moja kwa moja unaweza kufutwa mara moja. Wachangiaji wanaoleta uharabu kwa kusudi wanaweza kubanwa kwa muda fulani au milele na wakabidhi. Tendo la kumbana mchangiaji linapaswa kuelezwa angalau kifupi; kama ni kwa muda pia kwenye ukurasa wa majadiliano wa mhusika.
Ongeza michango chini ya mstari wa mwisho!