Majadiliano:Kitenzi

Kitenzi ni tendo lolote lililoweza kutendwa na mtu au kitu chochote chenye uwezo wa kutenda.Kwa ujumla maneno ambayo ni kitenzi yapo mengi katika lugha ya kiswahili. Kitenzi cha kiswahili kinabeba kiambishi kwa lengo la kuonyesha kazi mbalimbali za kitenzi hicho.Kazi hizo ni kama vile:nafsi,wakati,hali n.k.

Aina za kitenzi

hariri

Kuna aina tatu 3 za kitenzi ambazo ni :

  • (i)kitenzi kikuu (T)
  • (ii)Kitenzi kisaidizi(Ts)
  • (iii)Kitenzi kishirikishi (t)

(i)Kitenzi kikuu(T)

hariri

Ni aina ya kitenzi ambacho hubeba wazo kuu la sentensi.Kitenzi kikuu hukamilisha taarifa hata kikiwa peke yake.

(ii)Kitenzi kisaidizi(Ts)

hariri

Ni aina ya kitenzi ambacho huambatana na kitenzi kikuu katika kueleza tendo.Kitenzi kisaidizi hakiwezi kusimama peke yake na kutoa maana inayoeleweka mpaka kuwepo kitenzi kikuu.

(iii)Ktenzi kishirikishi(t)

hariri

Ni aina ya kitenzi ambacho huonesha uhusiano baina ya neno na neno.Kitenzi kishirikishi huweza kuonesha tabia au hali.

Rudi kwenye ukurasa wa " Kitenzi ".