Majadiliano:Methali

Latest comment: miezi 7 iliyopita by 105.161.197.82 in topic Polepole ndio mwendo

Waasalamu.Ningependa kupanua makala haya kwa kuchora Jedwali na kulipachika na methali za Kiswahili pamoja pengine na taafsiri zae za Kizungu na kisha kutoa maana/matumiza ya methali hiyo.Naomba ruksa au maoni yako.Ahsante.Limoke oscar (majadiliano) 08:23, 16 Aprili 2011 (UTC)Reply

Sina uhakika kama makala ya methali lazima iorodheshe methali nyingi. Hata makala ya Kiingereza inataja mifano michache tu. Kwa ajili ya kupata methali zenyewe, labda uwatafute waandishi wa Twitter, k.m. Swahili_Methali. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 10:19, 16 Aprili 2011 (UTC)Reply
Shikrani tele Baba Tabita.Labda nilikuwa natafakari mtu angependa kutaka kutambua maana au matumizi ya methali za Kiswahili na angeweza kupata makala hayo katika Wikipedia ya Kiswahili.Sijui waonaje hilo wazo?Limoke oscar (majadiliano) 10:40, 16 Aprili 2011 (UTC)Reply
Nichangie kidogo hapa. Kwa kawaida orodha ya methali ingekuwa jambo la Wikidondoo lakini hii hatuna bado kwa Kiswahili ukigonga "Wikidondoo" chini kwenye ukurasa wa Mwanzo unafikishwa Wikiquote ya Kiingereza. Kwa hiyo kwa sasa ninakubali kukusanya methali za Kiswahili hapa kwa mtazamo ya kwamba siku moja zitahamishwa Wikidondoo wakati tutakapopata tovuti hii. Kipala (majadiliano) 17:29, 19 Aprili 2011 (UTC)Reply
Kuna jambo au majambo kadha wa kadha. A) sioni sababu ya kuweka tafsiri ya Kiingereza ilhali hii ni Wikipedia ya Kiswaili. B) Sioni sababu ya kuweka mahli mahali pa mhariri wakati sehemu ya historia inaonesha nani aliyeandika. Ni lazima tufaute utaratibu wa kawaida. Ahsanteni sana.--MwanaharakatiLonga 15:03, 28 Aprili 2011 (UTC)Reply
Umesema! Kipala (majadiliano) 15:31, 28 Aprili 2011 (UTC)Reply

Methali

hariri

Methali ni semi fupi zenye mpangilio maalumu wa maneno ambazo hueleza kwa muhtasari,mafunzo na wazo zito linalotokana na uzoefu wa kijamii. Kimuundo methali huundwa kwa pande mbili ambazo upande wa kwanza huanzisha. Mfano.Haraka haraka-haina baraka

     Asiyesikia la mkuu-huvunjika guu
     Polepole-ndio mwendo
     Asiyefunzwa na mamaye-hufunzwa na ulimwengu

Methali hufanya kazi ya kuelimisha,kuonya,ushauli n.k.

Methalu

hariri

Polepole ndio mwendo 105.161.197.82 18:45, 26 Mei 2024 (UTC)Reply

Polepole ndio mwendo

hariri

Polepole ndio mwendo 105.161.197.82 18:47, 26 Mei 2024 (UTC)Reply

Rudi kwenye ukurasa wa " Methali ".