Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

  • usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
  • usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
  • usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
  • usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
  • do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Mr Accountable (majadiliano) 11:38, 24 Novemba 2009 (UTC)Reply

mbegu-jio-KE na mbegu-jio-Ethiopia

hariri

{{mbegu-jio-KE}} na {{mbegu-jio-Ethiopia}} ya kupatikana. --Mr Accountable (majadiliano) 17:45, 13 Desemba 2009 (UTC)Reply

Garissa

hariri

Rafiki OScar, nimerejesha makala ya Garissa. Una wajibu kuangalia kwanza kama makala iko tayari.

 
Onyo dhidi ya kuandika juu ya kazi ya wengine bila taarifa

Ulichangia makala katika wikipedia hii. Asante sana! Kwa bahati mbaya ulichagua kichwa kilichokuwepo tayari. Ukitumia google-translate labda hujatambua ya kwamba uliweka tafsiri yako juu ya makala iliyopo tayari.

Ni sawa kabisa ukibadilisha makala, au kuongeza mambo ndani yake.

Mara chache ni afadhali kufuta yote. Ila tu hapa kwenye wikipedia tunajadiliana kabla ya kufuta kazi ya wengine. Kuna ukurasa wa majadiliano unapoweza kutaja sababu kwa nini makala jinsi ilivyo si nzuri halafu subiri siku 2 hadi kufanya mabadiliko makubwa. Unaweza pia kiuangalia historia ya makala na kumwandikia mchangiaji aliyetangulia moja kwa moja.

Haikubaliki kufuta kazi ya wengine kimya-kimya. Hata kama hujakusudia kufanya hivyo tulilazimishwa kufuta kazi yako na kurejesha hali ya awali. Uko huru kuchukua sehemu za maandishi yako na kupeleka kama nyongeza katika makala iliyopo.

--Kipala (majadiliano) 19:25, 16 Desemba 2009 (UTC)Reply

Makosa

hariri

Salam, Limoke. Nimeona mara kadhaa ukiandika makala huku ukiwa umeacha vigezo au template za Wikipedia ya Kiingereza hapa kwenye Kiswahili - wakati vigezo vile havina kazi. Unaombwa uwe unaweka taratibu za kuondoa vigezo vyote vya Kiingereza - kwani havina kazi hapa kwenye Kiswahili. Pia, nimeona mara kibao ukiandika kiungo cha ndani cha Wikipedia huku ukiweka KOMA ndani yake. Hii haileti kiungo kwenda makala nyingine. Isitoshe, nimeona pia ukiweka hata NUKTA kwenye mabano mraba ya makala (mtu. badala ya mtu). Kumbuka kuondoa au kuepuka makosa haya, ndugu. Kila la kheri.--  MwanaharakatiLonga 10:10, 17 Desemba 2009 (UTC)Reply

Vigezo au Template

hariri

Ndugu, usiendelee kuanzisha vigezo bila kufahamu vina kazi gani, la. Ni lazima ufanya jambo ambalo unajua nini unachokifanya. Si vyema sana kuendelea kuanzisha vigezo bila kazi maalumu. Tafadhali unaombwa usiendelee kuanzisha vigezo, ndugu!--  MwanaharakatiLonga 13:31, 17 Desemba 2009 (UTC)Reply

Heri ya sikukuu

hariri

Salaam, Ndugu Limoke. Nimefurahi kuona kazi zako katika wikipedia yetu. Tuendelee kusonga mbele na kusaidiana. Heri ya sikukuu! --Baba Tabita (majadiliano) 10:08, 25 Desemba 2009 (UTC)Reply


makala zihitajizo habari

hariri

Ndugu Limoke, salaam! Wakati wa shindano, makala nyingi zimeanzishwa bila kuwekewa yaliyomo hata kidogo, nasi wanawikipedia hatukuwa na nafasi ya kurekebisha sana. Kwa hiyo sasa, naomba tusaidiane kusawazisha hizo makala. Kwa mfano, ungeweza kuanza kwa kuangalia orodha ya makala bila jamii. Bila shaka utagundua kadhaa ambazo ni duni, labda yenye maneno mawili matatu tu. Ndivyo nilivyogundua k.m. na makala ya Henri Fayol, mhandisi Mfaransa wa karne ya 19. Sasa ukiangalia mabadiliko niliyoyaingiza utapata mambo ya msingi ya wikipedia. K.m. naingiza kigezo cha {{DEFAULTSORT}} kwa ajili ya orodha ya makala katika jamii ifuate alfabeti vizuri. Tena naingiza jamii za miaka ya kuzaliwa (k.m. [[Jamii:Waliozaliwa 1841]]) na ya kufariki (k.m. [[Jamii:Waliofariki 1925]]). Pia, ikiwa ni makala fupi bila maelezo mengi, naingiza kigezo cha {{mbegu-mtu}} (yaani kama ni mtu). Hatimaye, naingiza kiungo kwa wikipedia ya Kiingereza (k.m. [[en:Henri Fayol]]) ambapo naweza kupata code kwa picha ya mtu (k.m. [[Image:Fonds henri fayol.jpg|thumb|right|Henri Fayol]]) pamoja na habari nyingine. Nitashukuru kwa msaada wako katika kuboresha makala mpya zilizoachwa duni. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 07:17, 3 Februari 2010 (UTC)Reply

nashukuru sana kaka,miye nitajitahidi kiasi niwezavyo koboresha makala ya wikipedia kwani miye ni mtumizi wa wiki kila siku kule chuoni wakati wote na nitafurahia sana japo mtu mwingine pia atapata makala yangu kuwa muhimu.Limoke

Ndugu Limoke, asante kwa jibu lako. Nimefurahi kusikia kuwa utaendelea. Unisamehe nikiendelea kuandika kuhusu usafishaji wa wikipedia baada ya shindano. Sababu hasa ni kwamba tukiendelea kuboresha makala zilizoongezeka, tuwe makini. Kabla hatujaongeza au kurekebisha habari za makala fulani, lazima tuangalie majadiliano na ukurasa wa historia ya makala hiyo. Angalia k.m. makala ya uchumi. Ukiihariri bila kuangalia majadiliano yake wala historia yake, inawezekana utaongeza kazi ya baadaye kwa vile tafsiri za shindano zilizofuta makala za zamani (pamoja na jamii na interwiki zake) hazijaunganishwa. Nitaendelea kutafuta makala kama hiyo na kuziandikia katika majadiliano yake. Kwa ajili ya kuunganisha tafsiri mbili au zaidi, labda itasaidia ukifungua zote, kila moja katika dirisha lake, na kunakilisha sehemu za makala za zamani kwenda katika makala ya sasa. Pole na kazi. Na asante kwa kazi yako. (Pia, ukiandika kwenye kurasa za majadiliano, ungeweza kutia sahihi kwa kutaipu ~~~~ ukiwa umesajiliwa kama Limoke oscar.) Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 04:08, 4 Februari 2010 (UTC)Reply


Ahsante sana Baba Tabitalakini miye bado nasumbuliwa sana na the technical bits za wiki,kama vile kuandika infobox,vigezo n.k. naomba sana kama ungeweza kunisaidia kidogo na kwanza nitaanza kwa kuboresha makala yangu binafsi kwa sababu nafahamu kuwa makala yenyewe sikuzingatia haswa kanuni za wiki.Miye Limoke oscar. Limoke oscar (majadiliano) 19:11, 14 Machi 2010 (UTC)Reply

~~~~ nimerudi sasa wanajumuia.kuanzia hii wiki,ni makala tuu.domo wazi nimewacha


Limoke oscar (majadiliano) 12:36, 16 Machi 2010 (UTC)Reply

Makala Baada ya Pambano la KWC

hariri

Nimeenza kutafsiri makala rasmi na kuandika makala.Hapa chini ni makala yangu ya kwanza tangu pambano liishe. Upper Nile, Sudan

Limoke oscar (majadiliano) 13:44, 16 Machi 2010 (UTC) Nimetumia Wiki Beta kuandika makala haya.Beta iko juu!Iko juu tu sana! Bukhungu StadiumReply

Haya, basijipongeze kwa matumizi yako ya Beta! Pia karibu tena katika Wikipedia ya Kiswahili. Uwepo wako utasaidia kuisukuma Wikipedia yetu kwa asilimi nyingi tu, kaka.--MwanaharakatiLonga 15:18, 16 Machi 2010 (UTC)Reply

Ahsante kaka User talk:Muddyb Blast Producer. Naomba msaada wenu ili niweze kuandika makala bora zaidi Nahisi kuwa bado sijahitimu kutosha kuandika makala bora ila naapa kujizitatiti.Miye Limoke oscar (majadiliano) 18:09, 16 Machi 2010 (UTC)18:05, 16 Machi 2010 (UTC)Reply

Sidhani kama kuna tatizo la kuto-kukusadia jinsi ya kuandika makala bora. Halafu sidhani kama kuna mmoja wetu anayeweza kusema makala fulani si bora! Ila tu, tunajitahidi. Basi jidhatiti ili tufikie lengo! Ukiwa una swali lolote kuhusiana na maujuzi au maujanja ya matumizi ya zana hizi za kiwiki, basi nijulishe nami nitakusaidia. Karibu sana.--MwanaharakatiLonga 06:25, 17 Machi 2010 (UTC)Reply

Nashukuru kaka User:Muddyb Blast Producer kwa wosia wako.Pia nasshukuru kwa kufuatilia makala yangu.Naomba ukiyakosoa uweze kuniaarifu ili niweze kupata kujibiresha hata zaidi katika nwiki.Nimetafsiri mengine.Limoke oscar (majadiliano) 08:16, 17 Machi 2010 (UTC)Reply


Ndugu Oscar kwanza kabisa karibu kwetu hata baada ya mashindano nakupongeza wa moyo wako wa kuendelea. Pili umeomba ushauri kuhusu makala ulizoaja hapo juu. Hapo naona kimsingi makala ya Upper Nile ni nzuri nitafirahi ukiendelea kuandika juu ya majimbo mengine ya Sudan pia. Kwa ushauri nina yafuatayo:
  1. Kusoma zaidi kidogo - yaani ukitangulia kusoma kwanza makala ya Sudan utaona majimbo yote ako tayari kwa viungo vya buluu maana mtu aliwahi kuunda makala; nikifungua naona ni mafupi sana sentensi moja tu zilianzishwa na mwenzetu Mr. Accountable ambaye anajua Kiswahili kidogo tu lakini anajitahidi kutusaidia sana. Makala hizi zote zinfaa kupanushwa.
  2. Jina: Kwa kusomasoma kidogo utaona jina la Kiswahili limeanzishwa tayari. "Upper Nile" inaweza kufaa kama kielekezo maana labda hata wasomaji wengine wanatafuta jina la KiingerEza katika wikipedia yetu, kielekezo itawapeleke huko. Napendekeza hatua zifuatazo: A) nakili na kuingiza maandishi ya Upper Nile kwenda "Nile ya Juu" halafu b9 badilisha yaliyomo ya Upper nile kuwa redirect kwenda kule Nile ya Juu.
  3. Kwa jumla tahadhari kidogo juu ya matumizi ya maneno ya Kiingereza. "White Nile" na "Scramble for Africa" zafaa kutafsiriwa. Hata hapa si vibaya kuchungulia katika wikipedia kama makala ziko tayari (Nile Nyeupe iko pekee kwa jimbo la Sudan; inaelezwa ndani ya makala ya mto Nile; mashindano ya wakoloni kugawa Afrika haina makala bado).
  4. wakati wa kutafsiri viungo kujiuliz: Je tunaitaka kweli? Yaani mimi ninsingetafsiri kiungo cha mafuriko ya Sudan 2007 kama nisingependa kuiandika mwenyewe; makalaet za Sudani ni kidogo sijui kama makala ii itakuja?
Basi haya ni mawazo machache tu naomba usikate tamaa na endelea!--Kipala (majadiliano) 09:28, 17 Machi 2010 (UTC)Reply

Shukrani Kaka Kipala,kidogo nina shida ya ku redirect vile umesema.unawez kunisaidia jinsi ya kufanya hivyo?Pili,nimetafsiri makal mengine haya hapa: Uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Moi na Western Stima.Pia naomba kujua jinsi ya kufuatilia wanawikipedia wengine ili nipate kuona jinsi wanavyo andika makala yao.Nimejaribu ku redirect vile umesema,makala ya hapo awali ndo haya Upper Nile, Sudan na mabadiliko ndo haya Jimbo la Nile ya Juu,Sudan shukrani.miye Limoke oscar (majadiliano) 11:25, 17 Machi 2010 (UTC)Reply

Redirect au kuelekeza si vigumu. Alama ya 12 juu ya dirisha la kuhariri ni #R. Baada ya kupeleka maandishi ya "Upper Nile" kwenda "Nile ya Juu" na kuhifadhi, unsrudi "Upper Nile". Bofya hariri, ondoa maandishi yote. Bofya alama ya Redirect #R utaona haya: #REDIRECT [[Insert text]]. Katika mabano mraba weka jina jipya yaani "Nile ya Juu". Hifadhi. Tayari. --Kipala (majadiliano) 11:29, 17 Machi 2010 (UTC)Reply
Nimeona, kumbe. Ulichofanya si vile ninavyoshauri. Yaani muhimu ni kusoma kwanza yale yaliyopo. Tusipate makala mbalimbali juu ya jambo moja kwa majina tofauti. Ukisoma "Sudan" utaona makala mebgu zote za majimbo ziko tayari, pamoja na kigezo (template). Makala hii iko kama mbegu kwa jina "Nile ya Juu". Ukipendelea majina tofauti (jinsi ulivyounda sasa) lazima ufuate kwa mbegu hizi zote za majimbo ya Sudan. Je ni lazima kweli? Sina neno lakini naona afadhali utumie yale yaliyopo ila tu ongeza habari ndani ya mebgu hizi fupifupi. --Kipala (majadiliano) 11:39, 17 Machi 2010 (UTC)Reply


Nimetafsiri na kuyakuza makala haya Waidakho kwenye Beta!Hee!Nafurahia Beta.16:32, 6 Aprili 2010 (UTC) Haya mengine ndo haya Francis Imbuga.Beta iko juu tu sana!Limoke oscar (majadiliano) 08:10, 7 Aprili 2010 (UTC)Reply


Limoke oscar (majadiliano) 11:42, 14 Aprili 2010 (UTC) Nafurahia kazi yangu Meja Mwangi!Nyingine tena kutoka kwa Limoke oscar (majadiliano) 11:42, 14 Aprili 2010 (UTC).Reply

Makala ya Waandishi wa Kenya

hariri

Nadhimiria kutafsiri na kuandika Makala haya.naomba msaada wowote.Mpmayenge (majadiliano) 09:09, 21 Aprili 2011 (UTC)Reply

Naona ni hoja zuri sana. Labda uanze kwa kutumuia en:Literature_of_Kenya? Haina habari nyingi lakini ni chanzo. Unaweza kuongeza habari za mitindo na kazi za waandishi na majina ya nyongeza polepole. Kipala (majadiliano) 12:25, 21 Aprili 2011 (UTC)Reply
Shukrani tele Kipala.Nitaendele basi.


Kiwix

hariri

Salaam Oscar, Oliver alinishauri niwasiliane nawe. Namhitaji mtu anayejua jinsi ganu Kiwix pamoja na wikipedia inaenda kwenye tovuti ya shule. Oliver alidhaniy a kwamba wewe ulihusika katika shule moja. Swali langu SI matumizi ya Kiwix ikiwekwa moja-moja kwenye kila kompyuta, bali matumizi yake ikiwa kwenye seva ya shule na wote wanaingia kupitia mtandao wa ndani. Je umewahi kuona hii? Kipala (majadiliano) 07:39, 13 Novemba 2012 (UTC)Reply

Waasalamu Kaka Kipala, nimeaannzisha mazungumzo na wasanidi wa Kiwix na pindi nipatapo jibu, nitakueleza. Ndivyo , matumizi yetu yalikuwa kwenye kila tarakilishi ya shule na bali sio kwenye seva. Limoke Oscar (majadiliano) 05:26, 15 Novemba 2012 (UTC)Reply